Hivi majuzi, mchezaji wa Brentford Ivan Toney alipigwa marufuku ya miezi minane na kupigwa faini ya milioni 8.5 baada ya kupatikana na makosa 232 yanayohusiana na kamari.
Ivan Toney sio mchezaji wa kwanza kuadhibiwa kwa makosa ya kamari; Sturridge, Trippier, Townsend ni miongoni mwa wachezaji wengine wa Ligi Kuu ambao waliwahi kupatikana na makosa kama hayo na kuadhibiwa vikali.