logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu mapendekezo ya mshahara wa Mbappe katika Al Hilal

Al Hilal imeandaa ofa nzuri ya mshahara kwa Mbappe huku wakisemekana kuwa tayari kumlipa bilioni 9.2 kwa mwezi.

image
na Samuel Maina

Habari25 July 2023 - 13:41

Muhtasari


  • •Al Hilal imewasilisha dau la pauni milioni 259 (Ksh 47.2B) kwa PSG ili kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe.
  • •Al Hilal imeandaa ofa nzuri ya mshahara kwa Mbappe huku wakisemekana kuwa tayari kumlipa bilioni 9.2 kwa mwezi.
Mapendekezo ya mshahara wa Mbappe Al Hilal

Klabu ya Saudi Arabia, Al Hilal imewasilisha dau la pauni milioni 259 (Ksh 47.2B) kwa PSG ili kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe.

Miamba hao wa Ufaransa ambao hawajakuwa katika uhusiano mzuri na mshambuliaji huyo wameripotiwa kukubali ombi hilo la kuvutia na kukubali kumuuza.

Hata hivyo, Al Hilal bado haijaanza mazungumzo na Mbappe mwenyewe kama ripoti kutoka Ulaya zinavyoonyesha. Iwapo nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa atakubali uhamisho huo, basi atakuwa mchezaji ghali zaidi wa soka wa wakati wote.

Al Hilal imeripotiwa kuandaa ofa nzuri ya mshahara kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 huku wakisemekana kuwa tayari kumlipa bilioni 9.2 kwa mwezi. Hii ni kumaanisha mchezaji huyo atakuwa anapokea mshahara wa takriban shilingi milioni 306.7 kwa siku, milioni 12.78 kwa saa na Ksh 212,986 kwa dakika moja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved