Tazama Wakenya mashuhuri na 'mapacha' wao wa kimataifa

Wakenya wengi wameshangazwa na mfanano mkubwa kati ya Betty Kyallo na mshambulizi Lauren James wa Uingereza.

Muhtasari

•Wakenya wamevutiwa na mshambulizi matata wa Uingereza, Lauren James ambaye wengi wanaamini anafanana sana na mwanahabari Betty Kyallo.

•Baadhi ya Wakenya wengine mashuhuri akiwemo waziri wa zamani Fred Matiang’i, mwanahabari Joshua Arap Sang, Njugush na wengine pia wamelinganishwa na mastaa wengine mashuhuri wa kimataifa.

Wakenya mashuhuri na 'mapacha' wao wa kimataifa
Image: ROSA MUMANYI
Wakenya mashuhuri na 'mapacha' wao wa kimataifa
Image: ROSA MUMANYI

Katika siku kadhaa za hivi majuzi, kipindi cha mashindano ya kombe la dunia ya wanawake yanayoendelea, macho ya Wakenya wengi yamevutiwa na mshambulizi matata wa timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza Lauren James ambaye wengi wanaamini anafanana sana na mwanahabari Betty Kyallo.

Wakenya wengi wameshangazwa na mfanano mkubwa kati ya Betty Kyallo na dada huyo na beki wa kulia wa Chelsea, Recce James.

Hapo awali, baadhi ya Wakenya wengine mashuhuri akiwemo waziri wa zamani Fred Matiang’i, mwanahabari Joshua Arap Sang, Njugush na wengine pia wamelinganishwa na mastaa wengine mashuhuri wa kimataifa.