Jinsi viongozi wa ODM walivyoadhibiwa kwa madai ya kukaidi msimamo wa chama

Chama cha ODM kilisema waliwaadhibu viongozi hao kwani walipinga maazimio yaliyotolewa na chama.

Muhtasari

•Jalang’o, Elisha Odhiambo, Gideon Ochanda, Caroli Omondi na Tom Ojienda wote walitimuliwa kutoka ODM kwa madai ya utovu wa nidhamu na kukaidi msimamo wa chama.

walivyoadhibiwa kufuatia mkutano wa NEC
Jinsi viongozi wa ODM walivyoadhibiwa kufuatia mkutano wa NEC
Image: WILLIAM WANYOIKE

Siku ya Jumatano, Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o na viongozi wengine wanne walifurushwa kutoka kwa chama cha ODM kufuatia mkutano wa cha wa NEC uliofanyika jijini Nairobi.

Jalang’o, Mbunge wa Gem Elisha Odhiambo, Mbunge wa Bondo Gideon Ochanda, Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi na seneta wa Kisumu Tom Ojienda wote walitimuliwa kutoka kwa chama hicho kinachoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu, Raila Odinga kwa madai ya utovu wa nidhamu na kukaidi msimamo wa chama.

Katika taarifa yake, chama cha ODM kilisema kuwa waliwatimua viongozi hao watano kwani walipinga maazimio yaliyotolewa na chama.

“Wanachama hao wanakabiliwa na tuhuma za ukiukwaji wa Ibara ya 11 (1) (e) ya katiba ya chama na kifungu cha 14A cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2011 kwa kujihusisha na kuunga mkono shughuli za chama pinzani na kupinga maamuzi/maazimio halali yaliyotolewa na chama. vyombo vya chama, wachukuliwe kama wamejiuzulu kutoka chama,” ilisomeka taarifa hiyo.

"Chama kinaagizwa kuanza mchakato wa kuwaondoa kwenye daftari la chama."

Mkutano wa NEC ulioitishwa na Raila mwenyewe ilikuja takriban mwezi mmoja baada ya wanachama hao kufika mbele ya kamati inayoongozwa na Sihanya kujitetea kutokana na shutuma za utovu wa nidhamu