Bei ya Petroli imepanda kwa jumla ya shilingi 52.52 tangu rais Ruto kuchukua hatamu

Mwezi Agosti mwaka jana Uhuru Kenyatta akiondoka madarakani, bei ya petroli ilikuwa shilingi 159.12 kwa lita.

Muhtasari

Hii ni mara ya tatu bei ya petroli kupanda kwa shilingi zaidi ya kumi kwa lita katika wakati mmoja.

Mwezi Septemba 2022 bei hiyo ilipanda kwa shilingi 20.18, Julai mwaka huu ikapanda kwa shilingi 13.49 na Septemba 15 imepanda kwa shilingi 16.96.

Bei za mafuta ya petroli.
Bei za mafuta ya petroli.
Image: william wanyoike,
bei za petroli,
bei za petroli,
Image: william wanyoike,