Tazama matukio muhimu katika ndoa ya Akothee na 'Omosh' tangu wafanye harusi

Akothee alifunga ndoa na Omosh mwezi Aprili, wakaenda kwa fungate mwezi Mei na hawajaonekana tena pamoja.

Muhtasari

•Matendo ya hivi majuzi ya Akothee kwenye mitandao ya kijamii yamewaacha wanamitandao  wakikisia huenda kuna tatizokwenye ndoa yake na Denis ‘Omosh’ Shweizer.

Matukio makubwa katika ndoa ya Akothee tangu harusi.
Matukio makubwa katika ndoa ya Akothee tangu harusi.
Image: ROSA MUMANYI

Mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee amekuwa akivuma katika kipindi cha siku mbili zilizopita baada ya kufunguka kuhusu masaibu yake vya kisaikolojia ambayo yalianza baada ya tukio ambalo hakufichua.

Baadhi ya matendo yake ya hivi majuzi kwenye mitandao ya kijamii yamewaacha wanamitandao Wakenya wakizungumza na kukisia kuwa huenda kuna tatizo fulani kwenye ndoa yake na Denis ‘Omosh’ Shweizer.

 Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 hata hivyo bado hajathibitisha au kukanusha tetesi za ndoa yake kuvunjika. Katika grafiki ya leo, tunakutembeza katika safari ya ndoa ya mwimbaji huyo na Bw Shweizer tukiangazia matukio makuu tangu harusi yao Aprili mwaka huu hadi matukio ya hivi majuzi.