Kiptum ,24, na kocha wake raia wa Rwanda Gervais Hakizimana walifariki papo hapo kufuatia ajali mbaya iliyotokea umbali mfupi sana kutoka kijiji chake cha Chepsamo, magharibi mwa Kenya.
Kiptum alivunja rekodi ya dunia ya marathon mwezi Oktoba, mwaka jana alipokimbia kwa masaa 2:00:35 katika Chicago Marathon, na kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia marathon chini ya saa mbili na dakika moja, na kuchukua sekunde 34 chini ya rekodi ya awali ya Mkenya mwenzake Eliud Kipchoge.