Fahamu mambo muhimu kuhusu muigizaji wa Nigeria Amaechi Muonagor na ugonjwa uliomuua

Sehemu ya mwili wa marehemu Muonagor ilikuwa imepooza kutokana na ugonjwa wa figo ambao umechukua maisha yake.

Muhtasari

•Amaechi Muonagor alithibitishwa kufariki  Jumapili, Machi 24  baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa figo kwa muda mrefu.

•Alifariki akiwa na umri wa miaka 62.

muhimu kuhusu Amaechi Muonagor na ugonjwa uliomuua.
Mambo muhimu kuhusu Amaechi Muonagor na ugonjwa uliomuua.
Image: WILLIAM WANYOIKE

Muigizaji Amaechi Muonagor alithibitishwa kufariki  Jumapili, Machi 24  baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa figo kwa muda mrefu.

Alifariki akiwa na umri wa miaka 62.

Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti kuwa mwigizaji huyo wa vichekesho alikuwa kwenye matibabu ya dialysis kabla ya kifo chake. Alikuwa amepooza kwa sehemu kutokana na ugonjwa wa figo ambao umechukua maisha yake.

Kifo cha muigizaji huyo mkongwe kimekuja siku chache baada ya video kusambaa ambapo alionekana akiomba msaada wa kifedha kutoka kwa Wanigeria ili kumwezesha kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya upandikizaji wa figo.