Vidokezo vya usalama kwa wanahabari wa kike wanapofuatilia habari kwenye maandamano

Baraza la vyombo vya habari nchini MCK limetoa tahadhari kwa waaandshi habari wa kike kuhakikisha wanavaa viatu vyepesi, visivyo wazi na visivyo na visigino virefu wakati wa kufuatilia maandamano.

Muhtasari

• Wanahabari wa kike wanashauriwa kutoweka maisha yao kwenye mkondo wa hatari wakati wa maandamano.

• Pia, MCK iliwashauri kutembea na firimbi au kengele za ubakaji ili kuwasaidia kupaza sauti endapo tukio la ubakaji au unyanyasaji wa kingono utakapojaribu kutokea kwao.

Vidokezo vya usalama wakati wa maandamano kwa waandishi wa habari wa kike
Vidokezo vya usalama wakati wa maandamano kwa waandishi wa habari wa kike
Image: HILLARY BETT