Jinsi Eldoret ilianza kama ‘Farm 64’ hadi kuwa jiji la 5 Kenya miaka 116 baadae
Eldoret ilianza kama makaazi ya jamii ya watu weupe wa Afrika Kusini, Boers ambao walikuwa wamependekeza mji huo kuitwa 'Girouard', jina la aliyekuwa gavana wa British East Africa wakati huo, Sir Percy Girouard.
Muhtasari
• Jina Eldoret lilipatikana kutokana na jina la Kimaasai 'Eldore' kuelezea hali ya mto Sosian uliokuwa na mawe mengi.