‘Abra K’ anachukua nafasi ya Rigathi Gachagia, aliyepewa jina la ‘Riggy G’ mwaka 2022 baada ya kuapishwa kama naibu rais.
“Profesa, kaka yangu mdogo, acha nikuite Abraham K ama Abra K. Karibu kwa huduma ya hili taifa la kipekee la Kenya. Na acha niseme hivi kwamba nimekusikia kwa hakika wakati ulikula kiapo chako, umesema kwamba utahudumia watu wa Kenya na taifa la Kenya. Abra K tafadhali, fanyia watu wa Kenya kazi na taifa la Kenya,” Ruto alisema.
Akimsisitizia, rais alisema kwamba wito wake ni ule ule kwa PS na CSs kwamba kila mmoja wao sharti ahudumie Wakenya na taifa kwa jumla na wala si kujihudumia.
“Kama ambavyo ninawaambia PSs na CSs, hatuko hapa kujihudumia wenyewe, au familia zetu, au maeneo tunako toka, tuko hapa kuhudumia Wakenya na taifa la Kenya,’ alisema.
Kindiki anachukua nafasi ya Gachagua aliyetimuliwa na seneti wiki mbili zilizopita kama naibu wa rais wa tatu chini ya katiba mpya ya Kenya ya 2010.