Gavana wa kaunti ya Trans Nzoia George Natembeya ametakiwa kufika mbele ya kamati ya habari, teknolojia na mawasiliano ICT ya bunge la seneti kujibu maswali kuhusu ukusanyaji wa kodi katika kaunti hiyo.
Seneta wa kaunti ya Nandi Samson Cherargei kwa niaba ya kamati hiyo, amesema hayo baada ya kuongoza mkutano na usimamizi wa kaunti ya Trans Nzoia inayoongoza mifumo ya ukusanyaji mapato kwenye kaunti ya hiyomjini Kitale mnamo Jumamosi Novemba 30.
Kwa mujibu wa seneta huyo, kaunti ya Trans Nzoia inayoongiozwa na aliyekuwa mratibu wa bonde la ufa George Natembeya, ina uwezo wa kukusanya mapato ya hadi shilingi bilioni 1.9 ikilinganishwa na shilingi milioni 500 inayokusanywa sasa. Shilingi hizomilioni 500 ni sawa na asilimia 25 ya uwezo wa kaunti hiyo kukusanya shilingi bilioni 1.9.
Katika mwaliko wa gavana Natembeya mbele ya kamati ya ICT ya seneti, atatakiwa kueleza kuhusu mfumo wa ukusanyaji mapato wa kaunti yake, utawala, utekelezwaji wa sheria pamoja na mapato ya chini yanayokusanywa kwenye kaunti hiyo.
Hata hivyo seneta Cherargei hajaweka wazi tarehe ambayo
gavana huyo anatarajiwa kufika mbele ya kamati anayoongoza.