Watu saba wamepoteza maisha yao na wengine kadhaa kupata majeraha kufuatia ajali ya barabarani ambayo imehusisha magari sita kwenye barabara ya Narok – Mai Mahiu katika eneo la Maltauro mchana wa Jumatatu Disemba, 23.
Kwa mujibu wa taarifa kuhusu tukio hilo, lori la masafa marefu lililokuwa likielekea upande wa Mai Mahiu likitoka Narok lilipoteza mwelekeo baada ya gurudumu kupasuka na kugonga magari mengine yaliyokuwa barabarani ikiwemo basi la abiria, gari ndogo la kibinafsi aina ya Premio na matatu ya abiria 14.
Muda mchache baadaye katika eneo hilo, trela nyingine iliyokujwa ikiend eshwa kwa mwendo wa kasi iligomgana na gari lingine la kibinafsi na kuwauwa watu wawili waliokuwa ndani ya Prado.
Wasafiri wawili waliokuwa ndani ya matatu katika tukio la kwanza walipoteza maisha hao katika tukio la ajali huku huku mwathiriwa mwingine akiaga dunia wakati alikuwa anapokea matibabu katika hospitali ya kaunti ya Narok.
Shirika la msalaba mwekundu limedhiibitisha tukio hilola
ajali kwenye mtandao wa X, likisema kwamba manusura waliopata ajali
wamekimbizwa katika hospitali ya Narok wanakopokea matibabu huku maafisa wa
usalama na wahudumu wa afya wa E-Plus wakiwa katika eneo la tukio.