Huduma ya kitaifa ya polisi kupitia ofisi ya inspekta jenerali Douglas Kanja hatimaye imetoa taarifa yake kuhusu madai ya maafisa wa huduma hiyo kuhusishwa na utekaji nyara wa vijana ambao habari za kupotea kwa vijana zaidi wa watatu katika muda wa wiki moja iliopita zimeenea kwenye mitandao za kijamii.
Katika taarifa iliyotiwa sahihi na Inspekta jenerali Douglas Kanja, taarifa hiyo imesema kuwa huduma ya polisi ina wasiwasi kuhusu taarifa zinazosambazwa na zinazohusishwa na idara hiyo ya maafisa wake kuhusika katika utekaji nyara wa raia ikisisitiza kuwa wajibu wa maafisa wake ni kukamata wahalifu ila si kuteka nyara.
IG Kanja amesema kuwa kuondoa shaka kwa Wakenya, huduma ya polisi ya kitaifa haijahusika katika utekaji nyara wowote na hakuna kituo chochote cha polisi nchini ambacho kinawazulia vijana wanaodaiwa kutekwa nyara.
“Ili kuepusha mashaka, huduma ya polisi ya taifa haihusiki na utekaji nyara wowote na hakuna kituo cha polisi nchini kinachowashikilia watuhumiwa hao.” Taarifa ya NPS ilisema.
Aidha huduma hiyo hata hivyo imeitaka umma kuepukana na usambaji wa habari za uwongo, uzushi, hasidi, karaha, taarifa zisizo sahihi na zisizothibitishwa kwa ajili ya kuichafulia sifa huduma ya kitaifa.
Hata hivyo mamlaka ya uangalizi wa utendakazi wa polisi nchini IPOA, mnamo Jumatano Disemba 25, kwenye taarifa yake ilisema kuwa uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na ongezeko la visa vya utekaji nyara vinavyodaiwa kufanywa na maafisa wa polisi.
Chini ya wiki moja iliyopita takribani vijana wanne
wameripotiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana katika kaunti za Embu,
Nairobi, Kajiado na Nandi.
IPOA hata hivyo imesema kuwa inachunguza utekaji
nyara wa Bill Mwangi, Peter Muteti Njeru, Benard Kavuli na mtu mwingine wa nne
ambaye angali kutambuliwa.