Hatimaye baada ya ngoja ngoja ya zaidi ya mwezi mmoja, sasa matokeo ya watahiniwa wa sekondari waliofanya mitihani ya kitaifa mwaka jana mwezi Novemba yametolewa.
Katika hafla ya kutangaza matokeo hayo iliyofanyika katika jumba la Mitihani, eneo la South C jijini Nairobi, waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba ametangaza matokeo hayo leo Alhamisi, Januari 6.
Ili kupata matokeo, wazazi wa watahinihiwa wameshauriwa kutembelea tuvuti ya baraza la kitaifa la mitihani au kutafuta matokeo kutumia uunganisho wa https://resultsKNEC.ac.ke kwa kuandika nambari ya kipekee ya usajili wa mwanafunzi kwenye tuvuti hiyo.
Aidha tuvuti hiyo imefunguliwa rasmi pindi tu baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo.
Matokeo ambayo yametolewa na baraza la kitaifa la mitihani KNEC, ni ya watahiniwa 965,501 waliokalia mtihani huo katika takribani vituo 10,755 kote nchini kuanzia Novemba mosi hadi Novemba 22.
Katika matokep hayo, watahiniwa mia nane na arubaini watakosa matokeo yao kutokana na visa vya udnaganyifu na matkeo yao yamefutiliwa mbali.
Watahiniwa wengine 2,829 watakosa matokeo yao kutokana na uchunguzi ambao unaendelea kufanywa kutokana na madai ya kuhusikakatika udanganyifu, Hatma ya wanafunzi hao
Vile vile watahiniwa hao ndio walifanya mtihani wa kitaifa wa shule ya msingi wakati wa virusi vya korona katika mwezi wa Machi mwaka wa 2022.
Waziri Ogamba ametangaza matokeo hayo siku chache baada ya
kutolewa kwa matokeo ya watahiniwa wa gredi ya 6 ambao pia walifanya tathmini
yao mwaka jana. Watahiniwa hao wa KPSEA wanatarajiwa kujiunga na sekondari msingi.