WHO yaomba Tanzania kutoa takwimu ya walioambukizwa corona

Muhtasari
  • WHO yaomba Tanzania kutoa takwimu ya walioambukizwa corona
  • Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, katika taarifa iliyoshirikiwa kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumapili, alielezea wasiwasi wake juu ya vifo vya hivi karibuni

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limetangaza tena wito kwa Tanzania kuweka mkabala njia  ya mapambano dhidi ya virusi vya corona.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, katika taarifa iliyoshirikiwa kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumapili, alielezea wasiwasi wake juu ya vifo vya hivi karibuni nchini humo vinavyohusishwa na maradhi hayo.

Wiki hii, Tanzania ilipoteza maafisa wakuu wawili wa serikali ambao wanasemekana walishindwa na COVID-19.

 

Wakati akiwafariji watanzania kufuatia kupoteza kwa maafisa wawili wa ngazi za juu serikalini, bosi wa WHO alisema hali ya COVID-19 katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki inapaswa kuzingatiwa sana.

Kulingana na Dkt Tedros, juhudi za WHO kusaidia Tanzania kupambana na Covid-19 kama nchi zingine zilikuwa zimepuuzwa.

“Mwishoni mwa Januari, nilijiunga na Dkt Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO katika Kanda ya Afrika, kuhimiza Tanzania kuongeza hatua za afya ya umma dhidi ya COVID-19 na kujiandaa kwa chanjo.

Nilihimiza pia kushiriki data kwa kuzingatia ripoti za visa vya COVID-19 kati ya wasafiri, ”inasema taarifa hiyo.

tangu wakati huo niliongea na mamlaka kadhaa nchini Tanzania lakini WHO bado haijapokea habari yoyote kuhusu hatua gani Tanzania inachukua kukabiliana na janga hilo."”inasema taarifa hiyo.

Mkuu wa WHO sasa anatoa wito kwa mamlaka ya Tanzania kuanza kuripoti kesi za COVID-19 na kushiriki data.

 Tedors alibaini kuwa Watanzania wanaosafiri kwenda nchi jirani na kwingineko wamepima Virusi vya covid-19.

 

"Hii inasisitiza hitaji la Tanzania kuchukua hatua madhubuti kuwalinda watu wao na kulinda idadi ya watu katika nchi hizi na kwingineko," alisema.

Tanzania iliacha kutoa takwimu za coronavirus mnamo Aprili mwaka jana kulikuwa na maambukizo angalau 509 na vifo 21.

Rais John Pombe Magufuli, ambaye mnamo Juni mwaka jana alitangaza Tanzania haina virusi kutokana na maombi "hivi karibuni aliwaonya watanzania dhidi ya kukumbatia chanjo" zisizo na ufanisi "za Covid-19 kutoka nchi za magharibi.

Alisema tiba ya mvuke imeonekana kuwa na ufanisi katika mapambano dhidi ya COVID-19 nchini.