Waziri wa Uganda apigwa risasi na watu wasiojulikana karibu na nyumba yake

Muhtasari
  • Waziri wa Uganda apigwa risasi na watu wasiojulikana karibu na nyumba yake

Jenerali Katumba Wamala, Mkuu wa zamani wa Jeshi la Uganda na Waziri wa sasa wa Ujenzi na Uchukuzi amepigwa risasi na kujeruhiwa na watu wasiojulikana karibu na nyumba yake katika mji mkuu Kampala.

Walioshuhudia wanasema watu hao wenye silaha walikuwa kwenye pikipiki.

Kwa miaka michache iliyopita, nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na mashambulizi kama hayo ya watu wenye silaha wanaoendesha pikipiki.

Mnamo Juni 2018, Ibrahim Abiriga, mwanasiasa shupavu na aliyekuwa mfuasi wa Rais Museveni alipigwa risasi na kuuawa karibu na nyumba yake. Andrew Felix Kaweesi wakati huo akiwa Mkuu wa Operesheni wa Polisi aliuawa kwa njia kama hiyo mnamo Aprili 2017. Hakimu na maulama kadhaa wa Kiislamu waliuawa vivyo hivyo.

Hakuna mauaji yoyote ambayo yamewahi kuchunguzwa kwa mafanikio au washukiwa kushtakiwa.

Jerali Wamala alikuwa mkuu wa jeshi la UPDF mwaka 2013 hadi 2017baadaye akapewa cheo cha waziri wa ujenzi na uchukuzi i na kwa wakati huu ni mmoja wa wabunge 10 wanaowakirisha jeshi la UPDF katika bunge la 11. Mwaka 2001 hadi 2005 alikuwa mkuu wa jeshi la polisi IGP.