Washukiwa katika shambulio la risasi dhidi ya Jenerali wa Uganda waonyeshwa kwenye CCTV

Muhtasari
  • Nitazidi kupigania maisha yangu, Jenerali Katumba azungumza baada ya shambulio
Image: BBC

Polisi nchini Uganda wametoa picha za mtaani za CCTV za wanaume wawili wanaoaminiwa kuhusika na jaribio la kumuua Waziri wa uchukuzi nchini humo.

Gari la Jenerali Katumba Wamala lilinyunyiziwa risasi na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki, na kumuua binti yake pamoja na dereva.

Inadhaniwa kuwa alikuwa akifuatwa na washambuliaji kwa mbali kabla ya shambulio la Jumanne.

Picha za video za CCTV zinawaonesha watu wawili. Mmoja wao amevalia fulana ya blu yenye mistari.

Moja ya pikipiki hizo iligeuza eneo ambalo sio mbali kutoka eneo la tukio la shambulio, kabla ya kutoweka ndani ya kituo cha petroli.

Hakuna hata sura ya mmoja wao inayoweza kutambulika.

Kikosi cha pamoja cha ujasusi cha polisi, na jeshi kinachunguza tukio hilo la ufyatuaji risasi.

Jeshi linasema linachunguza simu ambazo zinaonekana kuwa zilitumiwa kufanya mpango wa jaribio la mauaji.

Uganda imeshuhudia mashambulio kadhaa ya aina hiyo ya watu maarufu katika kipindi cha miaka michache iliyopita.

Huduma za ujasusi hazijaweza kutatua kisa chochote.

Kupitia kwenye ukrasa wake wa twitter jenerali huyo aliwashukuru wale wamekuwa wakimjulia hali na kutuma risala za rambi rambi kwa kumpoteza bintiye.