Rais Museveni aamuru kukamatwa kwa wanaosambaza uvumi kuwa amefariki

Muhtasari
  • Rais Museveni aamuru kukamatwa kwa wanaosambaza uvumi kuwa amefariki
Museveni
Rais Yoweri Museveni Museveni

Raia wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuna haja ya kuwakamata raia wa taifa hilo wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya.

Akizungumza na vyombo vya habari rais huyo ameshutumu wale wanaosambaza habari kwenye mitandao kwamba yeye amefariki.

Amesema kwamba wale wanaohusika na habari kama hizo wanapaswa kusakwa na kukamatwa kwa kuwa wamekuwa wakipotezea watu muda wao.

"Mitandao ya kijamii inaonekana imekuwa ikisema kuwa Museveni amekufa… tafuta haraka wale wanaosimulia hadithi kama hizo kwa sababu unapoteza wakati wa watu

Wengi sasa wanaitumia kueneza habari zisizo na msingi na zisizo na ladha na kuachana kabisa. Natoa wito kwa usalama kuangalia hii. Lazima isimamishwe, pata watu hawa, ” Museveni Alisema.

Hatahivyo akizungumza Rais Museveni alisema kwamba wale wanaozua habari kama hizo wanapaswa kufuatiliwa na vyombo vya usalama ili kukamatwa haraka iwezekanavyo.

Rais HUyo alizungumza siku ya Alhamisi alipokutana na wawekezaji wa nchi.