Msanii nyota wa Hip hop nchini Rwanda afariki ghafla

Muhtasari
  • Msanii nyota muziki wa Hip hop wa Rwanda Joshua Tuyishime al maarufu Jay Polly, amefariki ghafla katika hospitali jijini Kigali, kaka yake ameithibitishia BBC
Image: BBC

Msanii nyota muziki wa Hip hop wa Rwanda Joshua Tuyishime al maarufu Jay Polly, amefariki ghafla katika hospitali jijini Kigali, kaka yake ameithibitishia BBC.

Vyombo vya habari nchini humo zinasema kuwa Joshua Tuyishime alikimbizwa hospitalini kutoka gereza kuu laKigali baada ya kupatwa na ugonjwa usiojulikana Jumatano usiku.

Jay Polly mwenye umri wa miaka 33 alikamatwa mwezi Aprili kwa makossa ya matumizi ya dawa za kulevya, na kesi yake ilikuwa inaendelea.

Kaka yake Maurice Uwera amesema kuwa mamlaka ya huduma za magereza nchini Rwanda , “imeniambia”kuhusu kifo chake, lakini hakutoa maelezo zaidi.

RCS bado haijatoa maelezo kuhusu kifo cha nyota huyo wa muziki.

Mashabiki wengi wa muziki nchini Rwanda ambao walimfahamu Jay Polly kwa zaidi ya muongowamuziki wake wamekuwa wakitoa rambi rambi zao kupitia mitandao ya kijamii.