Guinea yafukuzwa kutoka Jumuiya ya ECOWAS kufuatia mapinduzi ya kijeshi

Uamuzi huo ulichukuliwa kufuatia mkutano uliofanywa kwa njia ya mtandao Jumatano.

Image: BBC

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS wameiondoa Guinea kutoka jumuiya hio kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya Jumapili ambayo yalimwondoa Rais Alpha Conde madarakani .

Uamuzi huo ulichukuliwa kufuatia mkutano uliofanywa kwa njia ya mtandao Jumatano. Kulingana na Reuters, uamuzi huo ulitangazwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Burkina Faso, Alpha Barry.

Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana ambaye pia ni mwenyekiti wa ECOWAS alisema kuwa mapinduzi ya kijeshi yalikiuka makubaliano ya jumuiya hiyo kuhusu utawala bora.

Umoja wa Afrika na ECOWAS wamelaani mapinduzi hayo ya kijeshi.