Wafahamu mawaziri wapya wa serikali mpya ya Taliban

Muhtasari

• Taliban waliitwaa Afghanistan kwa kipindi cha siku 10 pekee mwezi Agosti na mara moja wakachukua udhibiti wa miji mbali mbali, jambo lililowashtua watu wengi.

• Baraza la mawaziri linaongozwa na mmoja wa waanzilishi wa vuguvugu, Mullah Mohammad Hassan Akhund. Atahudumu kama Waziri Mkuu wa serikali ya mpito.

Image: AFGHAN ISLAMIC PRESS

Mawlawi Hibatullah Akhundzada ni mwanasiasa na kiongozi wa kidini wa tatu katika uongozi wa Taliban

Taliban waliitwaa Afghanistan kwa kipindi cha siku 10 pekee mwezi Agosti na mara moja wakachukua udhibiti wa miji mbali mbali, jambo lililowashtua watu wengi.

Kikundi hiki chenye silaha sasa kimetangaza majina ya awali ya mawaziri, na kugeuza jina la nchi kama "Milki ya Kiislamu."

Baraza la mawaziri linaongozwa na mmoja wa waanzilishi wa vuguvugu, Mullah Mohammad Hassan Akhund. Atahudumu kama Waziri Mkuu wa serikali ya mpito.

Wafuatao ni viongozi wakuu katika utawala wa sasa wa baraza la mawaziri la Taliban na taarifa zao muhimu tunazozijua kuwahusu

1. Hibatullah Akhundzada

Shibatullah Ahunzada alikuwa kiongozi wa ngazi ya juu zaidi wa Taliban mwezi Mei mwaka 2016 na sasa ndiye mkuu wa kile kinachoitwa Milki ya Kiislamu ya Afghanistan (Islamic Emirate of Afghanistan).

Katika miaka ya 1980, alishiriki katika vuguvugu la upinzani la Kiislamu na kupinga operesheni za kijeshi za Kisovieti , lakini wakati huo alijulikana zaidi kama kiongozi wa kidini kuliko kamanda wa jeshi.

Katika miaka ya 1990, Ahu Enzada alihudumu kama mkuu wa mahakama ya kidini ya kiislamu.

Walipoingia madarakani kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1990 , Taliban waliweka adhabu mbalimbali kwa misingi ya sheria ya Kiislamu -Sharia : Waliwanyonga wauaji na wazinzi hadharani na kuwakata viungo wezi.

Chini ya uongozi wa muasisi wa Taliban na kiongozi wa kidini Mullah Mohammed Omar (ambaye anaaminiwa kufariki mwaka 2013), Taliban pia walipiga marufuku televisheni, muziki, filamu na vipodozi, na waliwazuia wasichana wenye umri wa miaka 10 na zaidi kwenda shuleni.

Image: EPA

Inaaminiwa kuwa Ahu Enzada kwa sasa ana umri wa miaka 60 na zaidi na ameishi maisha yake zaidi nchini Afghanistan.

Hatahivyo kulingana na wataalamu, bado ana mawasiliano ya karibu na kile kinachitwa Quetta Shura. "Quetta Shura" ni shirika linalowajumuisha viongozi wa juu wa Taliban nchini Afghanistan. Wanasemakana wamekuwa katika mji wa Pakistan wa Quetta kwa muda mrefu.

Akiwa kamanda mkuu wa Taliban, Ahu Enzada ndiye mkuu wa masuala ya siasa, jeshi na dini.

2. Waziri Mkuu Minister-Mullah Mohammad Hassan Akhund

Mohamed Hassan Ahund ni mmoja wa watu walioanzisha Taliban nchini Afghanistan mwaka 1994.

Amekuwa kiongozi wa kamati maalum ya uongozi wa Taliban inayochukua maamuzi-Rehbari Shura kwa muda mrefu

Wakati Taliban ilipokuwa madarakani kuanzia mwaka 1996 hadi 2001, alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje na Naibu Waziri Mkuu.

Kwasababu ya cheo chake katika serikali wakati huo, kwa sasa amewekewa vikwazo na Umoaja wa Mataifa.

3. Waziri wa Mambo ya Ndani -Sirajuddin Haqqani

Haqqani ni kiongozi wa Mtandao wa Haqqani ambaye kikundi chake mnamo mwaka 2017, kilifanya shambulio la bomu lililotegwa ndani ya lori ambalo liligharimu maisha ya zaidi ya watu 150.

Mtandao wa Haqqani kwa sasa ni moja ya mashirika yenye silaha yanayoogopwa zaidi katika kanda hiyo. Baadhi ya watu wanasema kwamba kundi hilo hata lina ushawishi zaidi katika Afghanistan kuliko kundi linaloitwa Islamic State (IS).

Kikundi hiki pia kina uhusiano wa karibu na al-Qaeda. Marekani imeuorodhesha mtandao wa Haqqani kama "shirika la ugaidi."

Kulingana na maelezo ya FBI kuhusu mtandao wa Haqqani, ni kikundi kinachosakwa nan a shirika hilo.

Haqqani katika kitengo hiki kinatafutwa kuhojiwa kuhusiana na shambulio la 2008 dhidi ya hoteli mjini Kabul.

Shambulio hilo liliwauwa watu sita, akiwemo raia wa Marekani.

Image: FBI

Kikundi hiki kinaelezewa na Marekani kama shirika la ugaidi, lakini ndicho chenye jukumu la usimamizi wa fedha na mali za kijeshi za Taliban kwenye mpaka baina ya Pakistan na Afghanistan.

4. Naibu Waziri Mkuu -Abdul Ghani Baradar

Abdul Ghani Baradar ni mmoja wa waasisi wa Taliban.

Baada ya Taliban kupinduliwa na vikosi vya muungano vilivyoongozwa na Marekani mwaka 2001, alikuwa mtu muhimu katika kuwakuwasanya waasi.

Lakini mweiz Februali mwaka 2010, alikamatwa katika operesheni ya pamoja ya vikosi vya Marekani na Pakistan katika eneo la Karachi nchini Pakistan.

Image: GETTY IMAGES

Alifungwa jela miaka minane hadi alipoachiliwa baada ya kupangwa kwenye mchakato wa amani. Kuanzia Januari 2019, amekuwa mkuu wa kamati ya siasa ya Taliban huko Qatar.

Mnamo mwaka 2020, Baradar alizungumza na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kwa njia ya simu, na hivyo kuwa kiongozi wa kwanza wa Taliban kuzungumza moja kwa moja na rais wa Marekani.

Kabla ya hapo, Baradar alisaini makubaliano ya Doha kwa niaba ya Taliban, ambayo yaliahidi kuondoka kwa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan.

5. Waziri wa Ulinzi -Mohammad Yaqoob

Muhammad Yaqoob ni mtoto wa kiume wa Muhammad Omar, muasisi wa Taliban.

Inaaminiwa kuwa ana umri wa miaka 30 na zaidi na kwa sasa ni kamanda wa operesheni za kijeshi za Taliban.

Baada ya kifo cha kiongozi wa zamani wa Taliban Akhtar Mansour mwaka 2016, wanamgambo haohao walitaka kumteua Yaqoob kuwa kiongozi mpya wa juu zaidi wa Taliban lakini wengine walihisi kuwa alikuwa bado mdogo sana na hakuwa na uzoefu wa kutosha kuweza kuchukua wadhifa huo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Associated Press, wakati Taliban walipokuwa wakisonga mbele nchini humo, Jacob aliwataka wanamgambo wa Taliban kutowadhuru wanajeshi wa serikali ya Afghanistan, na kutochukua nyumba za maafisa wa serikali na usalama watakapotoroka.