logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Taliban wapiga marufuku unyoaji wa ndevu Afghanistan

Siku ya Jumamosi , wapiganaji wa kundi hilo, waliwapiga risasi na kuwaua watekaji wanne na miili yao kuzungunshwa katika barabara ya mkoa wa Herat.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri27 September 2021 - 06:11

Muhtasari


•Maagizo hayo yanasema kuhusu kurudishwa kwa sheria kali kama zile zilizokuwepo wakati kundi hilo lilipokuwa madarakani awali , licha ya ahadi ya kwamba litaanzisha serikali itakayokuwa na misimamo ya wastani.

•Siku ya Jumamosi , wapiganaji wa kundi hilo, waliwapiga risasi na kuwaua watekaji wanne na miili yao kuzungunshwa katika barabara ya mkoa wa Herat.

Kinyozi Afghanistan

Wapiganaji wa Taliban wamepiga marufuku , vinyozi katika mkoa wa Helmand nchini humo kutowanyoa au kuwapunguza ndevu wanaume, wakisema hatua hiyo inakiuka sheria ya Kiislamu.

‘’Mtu yoyote anayekiuka sheria hiyo ataadhibiwa’’ , Askari wa Taliban wamesema.

Baadhi ya vinyozi katika mji wa Kabul wamesema kwamba pia wao walipata maagizo kama hayo.

Maagizo hayo yanasema kuhusu kurudishwa kwa sheria kali kama zile zilizokuwepo wakati kundi hilo lilipokuwa madarakani awali , licha ya ahadi ya kwamba litaanzisha serikali itakayokuwa na misimamo ya wastani.

Tangu ilipochukua madaraka mwezi uliopita, Talibani imewapatia adhabu kali wapinzani wake.

Siku ya Jumamosi , wapiganaji wa kundi hilo, waliwapiga risasi na kuwaua watekaji wanne na miili yao kuzungunshwa katika barabara ya mkoa wa Herat.

Katika ilani iliochapishwa katika saluni, kusini mwa mkoa wa Helmand , maafisa wa Taliban walionya kwamba vinyozi lazima wafuate sheria ya Kiislamu katika kunyoa nywele za kichwani na ndevu.

Hakuna hata mtu mmoja aliye na uwezo wa kulalamika, ilisema notisi ilioonekana na BBC.

"Wapiganaji hao wanaendelea kuja na kutuagiza kutonyoa ndevu’’, alisema kinyozi mmoja mjini Kabul’.

Mmoja wao aliniambia kwamba wanaweza kutuma maafisa kuchunguza ili kutukamata. "

Kinyozi mwengine , ambaye anasimamia mojawapo ya saluni kubwa , alisema kwamba alipokea simu kutoka mtu aliyesema ni afisa wa serikali.

Walimtaka kutofuata mitindo ya Marekani na kutowanyoa watu ndevu zao. Wakati wa uongozi wa kwanza wa Taliban kuanzia 1996 hadi 2001, Kundi hilo lilipiga marufuku mitindo tofauti ya nywele na kusisitiza kwamba wanaume wafuge ndevu.

Lakini tangu wakati huo, unyoaji wa ndevu na nywele fupi miongoni mwa wanaume wa Afghan umekuwa maarufu.

Lakini baadhi ya vinyozi ambao hawakutajwa majina ili kuwalinda , wanasema kwamba sheria hizo mpya zinawapatia mazingira magumu ya kujipatia kipato.

‘’Kwa miaka mingi saluni yangu ilikuwa ikivutia vijana wadogo wanaotaka kunyolewa wanavyotaka ili kuonekana vijana wa kisasa’’, mmoja aliambia BBC. Hakuna haja ya kuendelea na biashara hii’’


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved