Wanandoa washtumiwa kutaka kuuza siri za manowari za kinyuklia

Muhtasari
  • Kulingana na taarifa hiyo, Bwana Toebbe na mpenzi wake sasa wameshtakiwa chini ya sheria ya atomiki
  • Bwana Toebbe alikuwa akifanya kazi katika mpango wa kinyukliana alikuwa ameidhinishwa na mpango wa usalama wa taifa hilo
Image: BBC

Jonathan Toebena mkewe Diana walikamatwa katika eneo la West Virginia siku ya Jumamosi , Idara ya haki ilitangaza .

Walidaiwa kujaribu kuuza muundo wa manowari ya kinyuklia, uliokuwa umefichwa katika sandiwichi kwa mtu waliyedhani alikuwa anawakilisha taifa jingine.

Mtu huyo alikuwa ajenti wa FBI.

Kulingana na taarifa hiyo, Bwana Toebbe na mpenzi wake sasa wameshtakiwa chini ya sheria ya atomiki.

Bwana Toebbe alikuwa akifanya kazi katika mpango wa kinyukliana alikuwa ameidhinishwa na mpango wa usalama wa taifa hilo.

Idara ya haki ilisema kwamba mnamo mwezi Aprili 2020, alituma kifurushicha data inayolindwa na ujumbe ulioonesha uhusiano fulani kwa serikali ya kigeni ili iiendelee kununua data kutoka kwake.

Baadaye alidaiwa kuanza kumuandikia mtu binafsi barua pepe ambayo ujumbe wake umefichwa.

Lakini wakati alipofikiria kwamba mtu huyo alikuwa akiwakilisha serikali ya kigeni , alikuwa afisa wa shirika la kijasusi la FBI .

Article share tools

  •  
  •