logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtoto aokolewa na paka Mumbai

Polisi wanasema wakaazi walimpata mtoto huyo baada ya kundi la paka waliokusanyika kando ya barabara na kuanza kuzua fujo - na kupiga kelele kwa sauti ya juu.

image
na Radio Jambo

Habari19 November 2021 - 04:57

Muhtasari


•Polisi wanasema wakaazi walimpata mtoto huyo baada ya kundi la paka waliokusanyika kando ya barabara na kuanza kuzua fujo - na kupiga kelele kwa sauti ya juu.

Mtoto wa kike wa siku tano, ambaye aliokolewa kutoka kwenye shimo la maji taka alimokuwa ametupwa jijini Mumbai, India anaendelea kupata nafuu katika hospitali ya eneo hilo.

Madaktari katika hospitali ya Rajawadi wameambia BBC kuwa "anaendelea vyema" na kwamba afya yake inafuatiliwa kwa karibu.

Polisi wanasema wakaazi walimpata mtoto huyo baada ya kundi la paka waliokusanyika kando ya barabara na kuanza kuzua fujo - na kupiga kelele kwa sauti ya juu.

Maafisa wanachunguza jinsi alivyoishia kwenye bomba hilo.

Polisi hawajatoa tamko lolote kuhusiana na kile kilochochangia tukio hilo lakini matukio mengine kama hayo siku za nyuma yamehusishwa na suala la watoto wa kiume kupendelewa zaii kuliko wa kike nchini India.

Wanawake mara nyingi wanabaguliwa kijamii na wasichana wanaonekana kama mzigo wa kifedha, haswa miongoni mwa jamii masikini.

Uwiano wa kijinsia wa nchi ni mojawapo ya hali mbaya zaidi duniani. Na ingawa mimba zinazokadiriwa kuwa za watoto wa kike hutolewa kwa usaidizi wa kliniki haramu, visa vya watoto wa hao kuuawa au kuachwa baada ya kuzaliwa si jambo la kushangaza.

Katika tukio la hivi punde zaidi, mtoto huyo aliokolewa na timu ya polisi inayoongozwa na wanawake kutoka kitongoji cha Mumbai siku ya Jumapili


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved