Aina mpya ya kirusi cha Corona yatua Ulaya

Muhtasari
  • Wataalamu mjini Geneva wataamua ikiwa kirusi hicho kinahitaji kutambuliwa kama ni hatari
Aina mpya ya kirusi cha Corona yatua Ulaya
Image: BBC

Ubelgiji imeripoti kisa cha kwanza cha aina mpya ya kirusi cha Corona barani Ulaya ambacho kwanza kigunduliwa nchini Afrika Kusini - huku Shirika la Afya Duniani likifanya mkutano maalum kuangazia umuhimu wake.

Wataalamu mjini Geneva wataamua ikiwa kirusi hicho kinahitaji kutambuliwa kama ni hatari.

WHO inasema itatoa mwongozo mpya baada ya mazungumzo lakini imeonya kwamba itachukua wiki kadhaa kubaini ikiwe kirusi hicho kivyoweza kuambukizwa na ikiwa chanjo itasalia kuwa na ufanisi dhidi yake.

Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen,iliwakumbusha watengenezaji kwamba kandarasi zao na EU inamaanisha lazima wabadili chanjo zao mara moja kwa kuzingatia kirusi hiki kipya.

Pia alisema kuwa safari zote za anga kwenda nchi zilizo na kirusi kipya cha corona zinapaswa kusitishwa.