Uchaguzi wa Gambia: Adama Barrow atangazwa kuwa mshindi kiti cha urais

Muhtasari

•Rais Barrow amepata takriban 53% ya kura za Jumamosi, huku mpinzani wake wa karibu - wakili, Ousainou Darboe – akiwa na kura 28%.

Rais mteule wa Gambia Adama Barrow
Rais mteule wa Gambia Adama Barrow
Image: AFP

Rais wa Gambia Adama Barrow ameshinda uchaguzi tena kwa urahisi, mamlaka nchini humo zimesema, katika kura zilizopigwa kwa mara ya kwanza kwa miongo kadhaa bila ya kiongozi wa muda mrefu Yahya Jammeh.

Rais Barrow amepata takriban 53% ya kura za Jumamosi, huku mpinzani wake wa karibu - wakili, Ousainou Darboe – akiwa na kura 28%.

Bw Darboe na wagombea wengine awali walisema hawakubaliani na matokeo ya uchaguzi huo.

Kura hizo zinaonekana kama jaribio la demokrasia nchini humo.

Katika uchaguzi uliopita, Bw Barrow alimshinda Yahya Jammeh, ambaye sasa anaishi uhamishoni baada ya kukataa kukubali matokeo.

Utawala wa miaka 22 wa Bw Jammeh uligubikwa na madai ya unyanyasaji, na mashahidi hivi karibuni waliiambia tume ya kuhusu wahusika wa utekelezaji wanavyoungwa mkono na serikali.

Licha ya uhamisho wake, Bw Jammeh bado ni mtu mwenye ushawishi mkubwa, alifanya kampeni akiwa mbali na kuwataka na kuwataka wananchi kutompigia kura Bw. Barrow.