Corona: Rais wa Msumbiji na mke wake wamejitenga

Muhtasari
  • Taarifa hiyo ilisema waliamua kufanya vipimo baada ya "shughuli walizokuwa nazo siku chache zilizopita 
  • Kumekuwa na ongezeko la virusi vya corona katika siku za hivi karibuni nchini Msumbiji
Rais wa Msumbiji na mkewe
Image: AFP

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na mke wake Isaura Nyusi wamekutwa na virusi vya corona na wamejitenga kwa sasa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya rais Bw. Nyusi na mke wake wameamua kujitenga kwa kuzingatia muongozo wa afya baada ya kupatikana na virusi , ijapokuwa hawakuonesha dalili zozote.

Taarifa hiyo ilisema waliamua kufanya vipimo baada ya "shughuli walizokuwa nazo siku chache zilizopita ".

Kumekuwa na ongezeko la virusi vya corona katika siku za hivi karibuni nchini Msumbiji.

Nchi hiyo imethibitisha kuwa na watu 193,000 wanaougua Covid-19, huku vifo 2,031 vikirekodiwa.