Papa Francis:Kuchagua kuwapenda wanyama badala ya watoto ni ubinafsi

Muhtasari
  • Papa Francis amependekeza kuwa watu wanaochagua kuwapenda wanyama zaidi ya watoto ni ubinafsi
  • Papa alizungumza hayo alipokuwa akijadili kuhusu suala la uzazi huko Vatican Roma
Pope Francis
Pope Francis
Image: Hisani

Papa Francis amependekeza kuwa watu wanaochagua kuwapenda wanyama zaidi ya watoto ni ubinafsi.

Papa alizungumza hayo alipokuwa akijadili kuhusu suala la uzazi huko Vatican Roma.

"Leo ... tunaona aina tofauti ya ubinafsi," aliwaambia . “Tunaona baadhi ya watu hawataki kupata mtoto.

"Wakati wengine wana mtoto mmoja tu, lakini wana mbwa na paka ambao huchukua nafasi ya watoto.

"Hii inaweza kufanya watu kucheka, lakini ndio uhalisia."

Kitendo hicho "ni kukataa kuwa baba na mama na kibaya, kinaondoa ubinadamu wetu", aliongeza.

Papa Francis alisema kwamba watu ambao hawawezi kupata watoto kwa sababu za kibaiolojia wanapaswa kuzingatia kuasili, na kuwataka watu "wasiogope" kuwa wazazi.

Pia alizungumza juu ya "msimu wa baridi huku idadi ya watu isiyotaka kupata watoto ikiongezeka - "tunaona kwamba watu hawataki kupata watoto zaidi na zaidi.".

Si mara ya kwanza kwa Papa Francis kulenga watu wanaochagua kuwapenda wanyama badala ya watoto.

Mnamo mwaka wa 2014, alisema kuwa na mapenzi na wanyama badala ya watoto lilikuwa "jambo jingine la uharibifu wa kitamaduni", na kwamba uhusiano wa kihisia na wanyama ulikuwa "rahisi" kuliko uhusiano kati ya wazazi na watoto