Kufutwa kazi kwa mwalimu anayenengua kiuno kwaibua mjadala kuhusu haki za wanawake Misri

Muhtasari

•Aya Yousef alifutwa kazi, na kutalikiana na mume wake , baada ya kuchukuliwa video na walimu wenzake kazini walipokuwa katika tukio la kijami kwenye boti mtoni Nile bila idhini yake.

Densi ya kungengua tumbo inasemekana kuanza tangu enzi ya Mafarao (picha ya maktaba)
Densi ya kungengua tumbo inasemekana kuanza tangu enzi ya Mafarao (picha ya maktaba)
Image: GETTY IMAGES

Nchini Misri, video ya mwalimu anayedensi kwa kunengua tumbo iliyosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii imeibua mjadala wa kitaifa kuhusu haki za wanawake na maadili ya kijami ya kihafidhina katika nchi hiyo.

Aya Yousef alifutwa kazi, na kutalikiana na mume wake , baada ya kuchukuliwa video na walimu wenzake kazini walipokuwa katika tukio la kijami katika boti kwenye mto Nile bila idhini yake.

Picha hizo zinaonyesha mwalimu huyo akionyesha umahiri wake wa kunengua kiuno akidensi pamoja mwalimu mwenzake wa kiume.

Densi ya kunengua tumbo inasemekanakuwa sehemu ya historia nchini Misri tangu enzi ya Mafarao , lakini kwa sasa wanawake wamekuwa wakizuiwa kuicheza hadharani.

Video ya Bi Yousef, ambaye anaonekana akiwa amevalia hijab na gauni lenye mikono mirefu kwa ajili ya safari ya mchana , inaonekana sio kitu cha aibu kwa viwango vya kimagharibi.

Hatahivyo, ilisambazwa sana kwenye mitandao ya habari ya kijamii katika kipindi cha wiki nzima iliyopita, na kuibua malalamiko makubwa miongoni mwa mahafidhina Wamisri.

Wakosoaji wake wanadai, alifanya kitendo cha aibu : "Inaelezea wazi nyakati duni tunazoishi!! Kila kitu kinaruhusiwa," aliandika mtumiaji mmoja wa Twitter.

"Elimu imefikia kiwango cha chini katika Misri ," mwingine alitoa maoni yake, huku akitoa wito wa uingiliaji kati wa mamlaka husika dhidi ya mwanamke huyo.

Bi Yousef alifutwa kazi na shule ya msingi alipokuwa akifundisha iliyopo katika eneo la Dakahlia katika Nile Delta, ambako alikuwa akifanya kazi kwa miaka kadhaa akifundisha domo la Kiarabu.

Ameapa kuwa hatawahi kudensi tena na alisema alijaribu kujiua katika kisa cha hivi karibuni kumuhusu .

"Dakika kumi katika boti katika mto Nile zimeyagarimu maisha yangu ," aliwaambia waandishi wa habari.

Wanawake watano walielezea hadithi yao ya kunyanyaswa kingono na unyanyasaji mwingine katika mazungumo na BBC idhaa ya Kiarabu (Oktoba 2018)
Wanawake watano walielezea hadithi yao ya kunyanyaswa kingono na unyanyasaji mwingine katika mazungumo na BBC idhaa ya Kiarabu (Oktoba 2018)
Image: BBC

Watetezi wa haki za wanawake nchini Misri pia waliongea kwa kauli kali, wakisisitiza kuwa mwalimuu huyo hakufanya kosa lolote na kusema kuwa alikuwea muathiriwa wa kampeni mtazamo wa kijamii.

Katika kumuunga mkono Bi Yousef na katika kutetea uhuru wa kibinafsi, Makamu mkuu wa shule nyingine alituma picha zake kwenye mitandao ya kijamii akidensi densi hiyo kwenye harusi ya binti yake.

Mkuu wa kituo cha Misri cha haki za wanawake Dkt Nihad Abu Qumsan, alimpatia ofay a kazi Bi Yousef katika ofisi yake na akamtaka alete mkataba wake kutoka wizara ya elimu ili kuwasilisha malalamiko ya kisheria dhidi ya kufutwa kwake kazi.

Hii huenda ilisaidia watu kufikiria upya. Maafisa sasa wamemteua Bi Yousef kuhamia katika shule nyingine.

Mwalimu alilalamika kuwa suala hilo lilikuwa ni "uingiliaji wa maisha yake ya kibinafsi ".

Alisema kuwa hakudensi katika taasisi ya umma au mbele ya wanafunzi na akasema alipanga kumshitaki mtu aliyechukua video hiyo mwezi uliopita.