Mlipuko mkubwa ulitokea katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumatano kwenye barabara inayoelekea uwanja wa ndege.
Kulingana na ripoti za Reuters baadhi ya miili ilikuwa ilionekana karibu na eneo la mlipuko. Mlipuko huo uliharibu magari manne na tuk tuk mbili.
Hadi wakati wa kuchapisha taarifa hii ilikuwa haijabainika kilichosababisha mlipuko huo.
Mhudumu wa afya alionekana akimhudumia angalau mtu mmoja aliyejeruhiwa.