Hali ya wasiwasi yazuka kuhusu Simba walioambukizwa Corona Afrika Kusini

Muhtasari
  • Wanasayansi hao wameonya kuhusu hatari ya kirusi kipya kutokea iwapo virusi hivyo vitasambaa katika hifadhi nyingine za Wanyama na kusambazwa tena kwa binadamu
Image: BBC

Simba na Puma katika mbuga ya kuhifadhia wanyamaporinchini Afrika Kusini huenda wameambukizwa virusi vya corona kutoka kwa wamiliki wao, kulingana na utafiti uliofanywa na wanasayansi katika chuo Kikuu cha Pretoria.

Wanasayansi hao wameonya kuhusu hatari ya kirusi kipya kutokea iwapo virusi hivyo vitasambaa katika hifadhi nyingine za Wanyama na kusambazwa tena kwa binadamu

Utafiti huo ulifanywa baada ya Wanyama hao kuugua na dalili ambazo zinafanana na zile za virusi vya corona kwa binadamu ikiwemo tatizo la kupumua , kutokwa na kamasi na kikohozi kikavu.

Vipimo vilivyofanyiwa Wanyama hao vilionesha kwamba wameambukizwa corona , watafiti hao walisema , huku data zikisema kwamba waliambukizwa ugonjwa huo na wafanyakazi waliokuwa wakiwahudumia.

Watafiti hao waliongezea kwamba wahudumu wa hifadhi hizo za Wanyama walikuwa na virusi vya corona walivyosambaziana wakati huo lakini hawakuonesha dalili zozote.

Wamependekeza hatua kama vile kuvalia barakoa wakati wanapowahudumia Wanyama hao.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la virusi la Peer Review