logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mzozo wa Ukraine: Watu 7 wafariki baada ya shambulio la bomu la Urusi

Watu 19 hawajulikani waliko

image
na Radio Jambo

Makala24 February 2022 - 08:18

Muhtasari


•Watu 19 hawajulikani waliko huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki katika Mariupol

Polisi wa Ukraine wakikagua mabaki ya kombora lililoanguka mtaani mjini Kyiv

Watu saba wanaaminiwa kufariki katika shambulio la bomu llililofanywa na vikosi vya Urusi, Polisi wa Ukraine wanasema.

Maafisa wanasema shambulio dhidi ya kambi ya jeshi ya Podilsk, nje ya mji wa Odessa liliwaua watu sita na kuwajeruhi wengine saba. Watu 19 hawajulikani waliko huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki katika Mariupol, waliongeza kusema.

Huku hayo yakijiri Wizara ya Ulinzi ya Urusi imenukuliwa na shirika la habari la Urusi -Interfax ikisema kuwa "Ulinzi wa anga wa vikosi vya jeshi la Ukraine umekandamizwa".

Wizara inaongeza kuwa "vikosi vya mpaka vya Ukraine havikupinga vitengo vya Urusi".

Hakujawa na uthibitisho huru wa madai haya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved