logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ukraine yadai kuwauwa wanajeshi 5,840 wa Urusi

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wanajeshi wake sasa wameuteka mji wa kusini mwa Ukraine

image
na Radio Jambo

Habari02 March 2022 - 11:32

Muhtasari


  • Jumla ya hasara ya Urusi inayodaiwa na Ukraine kufikia sasa ni pamoja na: Wanajeshi 5,840
  • Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wanajeshi wake sasa wameuteka mji wa kusini mwa Ukraine

Vikosi vya kijeshi vya Ukraine vimesema takwimu za awali zinaonesha vikosi vya kijeshi vya Urusi vimepata hasara kubwa tangu mwanzo wa uvamizi huo.

BBC haiwezi kuthibitisha madai haya kwa kina, lakini wizara ya ulinzi ya Uingereza inaamini kwamba vikosi vya Moscow vimepata hasara kubwa wakati wa uvamizi wake nchini Ukraine.

Jumla ya hasara ya Urusi inayodaiwa na Ukraine kufikia sasa ni pamoja na: Wanajeshi 5,840

- Ndege 30

-Helikopta 31

-Mizinga 211

-Magari 862 ya kivita (APVs)

- Tangi 60 za mafuta

-Magari 355

-Roketi 40 za MLRS (zilizokamatwa)

KATIKA HABARI HIZO ZA MZOZO WA UKRAINE IN KUWA;

Urusi yadai kuudhibiti mji wa Kherson

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wanajeshi wake sasa wameuteka mji wa kusini mwa Ukraine wa Kherson.

Ikiwa mji huo umedhibitiwa na Urusi, utakuwa mjini mkubwa zaidi nchini Ukraine kudhibitiwa na vikosi vya Urusi hadi sasa.

Usiku wa kuamkia leo tuliripoti kuwa wanajeshi wa Urusi walionekana katika mitaa ya mji huo na kwamba meya wake alisema kituo cha treni cha Kherson na bandari vimetekwa.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved