Vijana Zimbabwe watumia taulo za kike na nepi za mkojo za watoto kama 'kilevi'

Muhtasari

• Wanapata dutu nyeupe au kemikali inayojulikana kama sodium polyacrylate - kutoka kwa bidhaa hizi na kuichemsha.

Image: Getty Images

Baadhi ya vijana nchini Zimbabwe wanaripotiwa kuchukua kemikali zinazotumika kwenye nepi na taulo za kike 'pedi' na kuzitumia kama kilevi cha bei nafuu.

Wameiambia Al Jazeera kwamba wanapata dutu nyeupe au kemikali inayojulikana kama sodium polyacrylate - kutoka kwa bidhaa hizi na kuichemsha. "Baada ya kuchemsha, huunda dutu ya kijivu na tunakunywa mchanganyiko huo," kijana mwenye umri wa miaka 19 aliiambia Al Jazeera.

Kemikali hiyo ndiyo inayotumika kunyonya damu ya hedhi kwenye taulo za kike 'pedi' na mkojo kwenye nepi za watoto 'diapers'. Inayeyuka mara moja inapochemshwa.

Matumizi mabaya ya dawa za kulevya na utumiaji wa njia mbadala za vijana kujiinua inatupiwa lawama kutokana na kukosekana kwa mitandao ya usalama wa kijamii nchini Zimbabwe huku kukiwa na uchumi duni.