Elena Kabayeva: Mfahamu mke wa siri wa Rais Vladimir Putin ni nani?

Muhtasari

Kulingana na Jarida la Wall Street, Marekani inapanga kuwawekea vikwazo "marafiki" wa Putin, lakini hilo halikufanyika katika dakika za mwisho.

 

Elena Kabayeva,
Elena Kabayeva,
Image: SASHA MORDOVETS / GETTY IMAGES

Elena Kabayeva, anajulikana kama "Mama taifa wa kisiri" nchini Urusi. Ameangaziwa tangu Urusi ilipovamia Ukraine.

Hii ni kwa sababu Marekani iliwawekea vikwazo wandani wa karibu wa Rais Vladimir Putin, wakiwemo mabinti zake. Lakini kufikia sasa hakuna vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Elena.

Kulingana na Jarida la Wall Street, Marekani inapanga kuwawekea vikwazo "marafiki" wa Putin, lakini hilo halikufanyika katika dakika za mwisho.

Inadhaniwa kwamba endap hilo lingetokea, Putin angelichukulia hatua hiyo kama shambulio la kibinafsi dhidi yake mwenyewe na lingeweza kuvuruga juhudi za amani.

Hata hivyo Katibu wa Habari wa Ikulu ya White House Jane Sackie siku ya Jumatatu alikanusha kwamba Marekani haikuwa imemwekea vikwazo mwanamke huyo, ambaye anasemekana kuwa mwandani wa karibu wa Rais wa Urusi.

Alipoulizwa kwa nini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya mshindi huyo wa zamani wa medali ya dhahabu ya Olimpiki, alijibu kwamba Marekani ilikuwa ikizingatia kwa uzito vikwazo.

Putin na Elena
Putin na Elena
Image: REUTERS

Elena Kabayeva ni nani?

Elena alishinda medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya Athens mwaka wa 2004. Alianza kufanya mazoezi akiwa na umri wa miaka 13 na kupata ushindi wake wa kwanza wa dunia mnamo 1998.

Tangu wakati huo ameshinda medali kadhaa zikiwemo za Mashindano ya Uropa ya 2001 na 2002. Pia alishinda Makombe kadhaa ya Dunia mnamo 2003.

Elena alijiunga na siasa za Urusi mwaka 2005, jina lake lilipohusishwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Pia alichaguliwa kuingia katika Duma, nyumba ya chini ya bunge la Urusi. Mnamo 2014, alitunukiwa kuwa mmoja wa wanariadha kadhaa waliobeba mwenge wa Michezo ya Olimpiki ya Sochi.

Image: GETTY IMAGES

Elena kando na kujihusisha na michezo na siasa, pia amekuwa mkuu wa vyombo vya habari vya kitaifa vya Urusi. Kulingana na gazeti la Moscow Times, jina lake liliondolewa kwenye tovuti baada ya kuwa wazi mwezi Aprili kwamba vikwazo vya Magharibi vinaweza kuwekwa kwa sababu ya vita vya Ukraine.

Aidha kulingana na gazeti hilo la Moscow Times, maafisa kutoka Iswizi, Marekani na Ulaya ziliambia Jarida la Wall Street kwamba Elena alisafiri Uswizi mwaka 2015 kwenda kujifungua. Mwaka 2019, Elena alijifungua mapacha mjini Moscow. Lakini Rais Putin hajawahi kuthibitisha hili.

Ushiriki wake katika Tamasha la Moscow

Kulingana taarifa katika gazeti la Moscow Times, Elena Kabayeva wiki iliyopita alihudhuria sherehe katika mji mkuu wa Urusi. Alikuja kwa onyesho la mazoezi, ambalo litatolewa Siku ya Ushindi wa Urusi mnamo Mei.

Image: GETTY IMAGES

"Kila familia ina hadithi ya kusimulia, na tusisahau kuisimulia kwa vizazi vijavyo," alisema.

Alisema anaunga mkono Muungano wa Marekani, lakini kudumisha uhuru ni muhimu kwa Urusi.

Kulingana na Daily Mail, baada ya ushiriki wa Elena katika mpango huo, uvumi ulienea kwamba alikuwa amejificha kwenye ghala huko Uswizi au Siberia.

Mamia ya watoto walihudhuria sherehe hiyo, ambayo pia ilikuwa na nembo ya 'Z', ishara ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO.