Mwanamke afungwa miaka 20 kwa mauaji ya mwanawe aliyekuwa anaugua maradhi ya pumu

Muhtasari

•Hakeem Hussain mwenye umri wa miaka saba alifariki nyumbani kwao huko Birmingham mnamo Novemba 2017.

•Usiku ambao Hakeem alikufa, mamake alikuwa amevuta heroine kabla ya kuzimia katika kitanda kimoja naye.

Uraibu wa Laura Heath wa dawa za kulevya ulikuwa mbaya zaidi katika miezi iliyotangulia kifo cha Hakeem, mahakama ilifahamishwa
Uraibu wa Laura Heath wa dawa za kulevya ulikuwa mbaya zaidi katika miezi iliyotangulia kifo cha Hakeem, mahakama ilifahamishwa
Image: WEST MIDLANDS POLICE

Mama wa mvulana aliyepatikana akiwa amefariki kwenye bustani yenye baridi kali baada ya shambulio la pumu amefungwa jela miaka 20.

Hakeem Hussain mwenye umri wa miaka saba alifariki nyumbani kwao huko Birmingham mnamo Novemba 2017.

Mahakama ilifahamishwa kwamba Laura Heath alikuwa ametanguliza uraibu wake wa dawa za kulevya kuliko kumtunza mwanawe.

Mama huyo wa miaka 40 alipatikana na hatia ya kuua bila kukusudia baada ya kukiri makosa manne ya ukatili dhidi ya mtoto katika Mahakama ya Coventry Crown.

Mahakama ilisikia kuwa Hakeem, ambaye anajulikana na mamlaka, alikufa peke yake "akijaribu kuvuta pumzi" katika bustani ya sehemu mama yake alikuwa akiishi.

Uraibu wake wa dawa za kulevya ulikuwa mbaya zaidi katika miezi iliyotangulia kabla ya kifo cha mwanawe, kiasi ambacho alikuwa akilipa pauni 55 kwa siku kupata heroine na cocaine, ambayo alilipwa kwa kiasi fulani kupitia kazi ya ngono.

Jaji pia aliambiwa kuwa alikuwa ametumia tena kipulizia chake kama bomba la kupasuka kwa muda.

Usiku ambao Hakeem alikufa, Heath alikuwa amevuta heroine kabla ya kuzimia katika kitanda kimoja naye.

Huenda kwa kuchochewa na madhara ya moshi wa sigara, Hakeem wakati fulani mwendo wa usiku alipata shambulio la pumu.

Hakuweza kumwamsha mama yake, inadhaniwa kisha akatoka nje ili kupata hewa safi, ambapo alipatikana asubuhi iliyofuata, akiwa bado ameshika jani.

Mwili wa Hakeem Hussain ulipatikana kwenye bustani yenye baridi kali mwezi Novemba 2017
Mwili wa Hakeem Hussain ulipatikana kwenye bustani yenye baridi kali mwezi Novemba 2017
Image: FAMILY

'Ufukara, machafuko na janga'

Akitoa hukumu dhidi ya Heath, Jaji Dove alisema kifo cha Hakeem kilitokana na malezi ya Heath katika "mazingira ya kusikitisha".

Kifo cha Hakeem kilitokea baada ya maisha yake " kusambaratika kutokana na matumizi wa dawa za kulevya katika hali ya ufukara, machafuko na janga," alisema.

Mvulana huyo aliishi katika mazingira ya kusikitisha

"Ni wazi kwamba katika maisha yake mafupi ya kuhuzunisha [Hakeem] amekuwa na furaha na upendo kwa watu waliomfahamu," Jaji Dove alisema.

"Uwezo huo wote wa maisha mazuri na yakuridhisha ulikatizwa, baada ya kuanguka kwa kukosa hewa, na kufa akishikilia jani kwenye bustani.

"Ukweli ni kwamba Hakeem alikufa kwa sababu ya uzembe wako."

Kifo chake "hakikustahili kutokea, kilitokana na sababu ya kusikitisha na na uzembe wako kama mama yake", hakimu alisema.

Uchunguzi wa maiti ulithibitisha kwamba Hakeem alikufa kwa pumu ambayo haikudhibitiwa, na kipimo cha sumu kilithibitisha alikuwa amevuta moshi wa tumbaku saa chache kabla ya kifo chake.

Sampuli ya nywele ilionesha pia alikuwa ametumia heroine, cocaine na bangi.

Hakeem alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kupumua na pumu tangu akiwa na umri wa miaka mitatu na mamlaka ilikuwa na wasiwasi kuhusiana na hali yake ya afyana jinsi alivyokuwa akishughulikiwa nyumbani, mahakama iliambiwa.

Wakati wa kifo chake, hakuweza kupata kipulizia chake kwa siku mbili kwa sababu mama yake hakuenda kumchukulia.

Onyo imetolewa mara kadhaa kuhusu usalama wa Hakeem katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Siku mbili tu kabla ya mwili wake kupatikana, muuguzi katika shule yake aliambia jopo la ulinzi kuwa atakufa "ifikapo wikendi" ikiwa hatua hazitachukuliwa.

Mahakama ilifahamishwa kwamba wakati wa mkutano wa Ijumaa kabla ya kifo chake, afya, elimu, na wafanyakazi wa kijamii walipiga kura kuchukua hatua kumlinda Hakeem, na mazungumzo na Heath yalitarajiwa kufanyika baada ya wikendi.

Hakeem alifariki siku ya Jumapili.

Uchambuzi

Wakati wa kifo cha Hakeem, Huduma ya Watoto ya Birmingham ilikuwa tayari imekadiriwa kuwa mapungufu kwa takriban muongo mmoja, wakati ambapo zaidi ya watoto 12 waliotambuliwa na mamlaka kuwa wanatelekezwa walikufa, ikiwa ni pamoja na Khyra Ishaq wa miaka saba, ambaye alikufa kwa njaa, wawili- Keanu Williams mwenye umri wa miaka, ambaye aliuawa na mama yake na Keegan Downer, mwenye umri wa miezi 18, ambaye mlezi wake alimuua.

Miezi sita baada ya Hakeem kufariki, kundi jipya la wadhamini liliteuliwa kuchukua wadhifa huo, na tangu wakati huo ukaguzi umeonyesha kuwa mambo yameboreka.

Tathmini ya kina kuhusu kifo cha Hakeem itachapishwa ndani ya miezi miwili ijayo, lakini mifumo mipya tayari imewekwa ili kusaidia kupunguza hatari ya kifo kingine kama cha Hakeem.

Khyra Ishaq, Keanu Williams na Keegan Downer walikuwa miongoni mwa zaidi ya watoto12 waliotambuliwa na mashirika ya Birmingham kwamba wanatelekezwa kabla ya vifo vyao.

Shirika la kuhudumia watoto la Birmingham lilisema "fursa ya kumuokoa" ilipotezwa na wafanyikazi wa kijamii katika kesi ya Hakeem.

Mtendaji wake mkuu, Andy Couldrick, alisema: Hakeem "alikuwa akiwaambia baadhi ya watu hali aliyokuwa akipitia lakini hakuna aliyetilia maanani kando na kumsikitikia na kumsaidi mara kwa mara".