Tanzania yakanusha madai ya utekaji nyara katika mbuga ya Serengeti

Muhtasari

•Watu kadhaa wanadaiwa kutoweka miezi kadhaa baada ya kukamatwa katika hali isiojulikana na wale wanaodaiwa kuwa maaskari wa mbuga hiyo.

Image: BBC

Shirika la mbuga za kitaifa za wanyapori nchini Tanzania limekana ripoti kwamba maafisa wake waliwanyanyasa na kuwateka wakaazi katika mbuga ya wanyamapori ya Serengeti.

Hatua hiyo inajiri kufuatia madai kwamba baadhi ya watu wametoweka miezi kadhaa baada ya kukamatwa katika hali isiojulikana na wale wanaodaiwa kuwa maaskari wa mbuga hiyo.

Katika taarifa , Shirika la kitaifa la mbuga za wanyamapori nchini Tanzania Tanapa , limesema kwamba halijapokea ripoti zozote zilizo rasmi kuhusu unyanyasaji huo uliotekelezwa na askari wa Wanyama pori wala ripoti kuhusu raia waliodaiwa kutoweka.

Iliwashauri wale wanaomiliki mitandao ya kijamii kuthibitisha habari wanazopokea ili kutosababisha hali ya wasiwasikuhusu masuala yanayohusu maisha ya binadamu.

Tanapa imesema kwamba itaendelea kuchukua jukumu lake la kuhifadhi mbuga za Wanyama pori za taifa hilo.