Ndege yarudishwa ikiwa angani baada ya rubani kubainika hajakamilisha mafunzo

Muhtasari

•Ndege ya Virgin Atlantic ilirejeshwa katika uwanja wa Heathrow baada ya hitilafu ya orodha ya majaribio kwa rubani wa ndege hiyo ya Virgin Atlantic ambayo likuwa ikielekea New York

Image: GETTY IMAGES

Ndege ya Virgin Atlantic ilirejeshwa katika uwanja wa Heathrow baada ya hitilafu ya orodha ya majaribio kwa rubani wa ndege hiyo ya Virgin Atlantic ambayo likuwa ikielekea New York.

Ilibainika kuwa afisa wa kwanza hakuwa amekamilisha mtihani wake wa mwisho wa kuruka.

Takriban dakika 40 za safari ya ndege kuelekea New York siku ya Jumatatu, marubani hao wawili walifahamu "kosa la uorodheshaji", shirika hilo la ndege lilisema.

Ndege ya VS3 ilikuwa imefika angani juu ya Ireland kabla ya kurejea Heathrow. Virgin Atlantic ilisema mtu aliyechukua nafasi ya afisa wa kwanza alipatikana na ndege ikaondoka tena kuelekea New York.

Shirika hilo la ndege lilisisitiza usalama haukuathiriwa na kuelezea afisa wa kwanza alijiunga na Virgin Atlantic mnamo mwaka 2017.

Alikuwa amehitimu kikamilifu chini ya kanuni za usafiri wa anga za Uingereza, shirika hilo la ndege liliongeza, lakini hakuwa amekamilisha safari ya mwisho ya tathmini ambayo ilikuwa sehemu ya mahitaji ya ndani ya shirika hilo. Ndege ilirudi nyuma kwani nahodha hakuwa ameteuliwa kuwa mkufunzi.

Udhibiti wa ndege kwa kawaida hushirikiwa kati ya afisa wa kwanza, lakini wa pili huwa na jukumu la mwisho kwa kile kinachotokea kwenye ndege.

Msemaji wa Virgin Atlantic alisema: "Afisa wa kwanza aliyehitimu, ambaye alikuwa akisafiri kwa ndege pamoja na nahodha mwenye uzoefu, alibadilishwa na rubani mpya ili kuhakikisha utiifu kamili wa itifaki za mafunzo za Virgin Atlantic, ambazo zinazidi viwango vya tasnia.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa wateja wetu ambao walifika saa mbili na dakika 40 kuliko ilivyopangwa kutokana na mabadiliko ya wafanyakazi. Msemaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (CAA) alithibitisha marubani wote wawili walikuwa na leseni ifaayo na "wamehitimu kufanya safari".