logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tumbili aiba ushahidi muhimu kwenye kesi ya mauaji mahakamani

ushahidi huo ni pamoja na kisu kinachoaminika kutumika katika mauaji hayo.

image
na Radio Jambo

Habari12 May 2022 - 10:04

Muhtasari


•Inaripotiwa ushahidi ulioibiwa na tumbili huyo ni pamoja na kisu kinachoaminika kutumika katika mauaji hayo.

Kesi ya mauaji ya mwaka 2016 nchini India imeahirishwa baada ya polisi kusema ushahidi uliokusanywa uliibiwa na tumbili.

Gazeti la The Times of India linaripoti kwamba ushahidi ulioibiwa na tumbili huyo ni pamoja na kisu kinachoaminika kutumika katika mauaji hayo.

Polisi wa Jaipur wametuma barua kwa mahakama wakisema tumbili huyo alitoroka na ushahidi huo alipokuwa akielekea kwenye hifadhi.

Mahakama tayari imewataka polisi kuwasilisha ushahidi katika kesi ya mauaji ya Shashikant Sharma, ambaye alipatikana amefariki miaka sita iliyopita karibu na Kituo cha Polisi cha Chandwaji huko Jaipur.

Polisi walisema katika taarifa kwamba afisa huyo alikuwa amepumzika chini ya mti, kisha tumbili huyo akanyakua ushahidi huo na kutoweka.

Ghasia zilizuka baada ya siku kadhaa za mauaji ya Shashikant Sharma huko Jaipur, na polisi baadaye waliwakamata wanaume wawili, Rahul na Mohanlal Kandera, kutoka jiji hilo.

Mwendesha mashtaka pamoja na hakimu wa mahakama hiyo wanasemekana kughadhabishwa na uzembe wa polisi wa Jaipur, na wanasema hoja kwamba ushahidi kwamba uliibiwa na tumbili huyo si wa kawaida.

Haijulikani atafanya nini baada ya kuacha wadhifa huo.

Tukio lingine la kushtua lilitokea nchini India mwishoni mwa mwaka jana, baada ya maafisa kusema kuwa wamekamata nyani wawili kwa kuua karibu mbwa 250.

Shambulio hilo lilielezewa na Huduma ya Misitu ya India kama kulipiza kisasi kwa mauaji ya tumbili na mbwa


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved