Mzozo wa UKraine: Mjane wa Ukraine amkaripia mwanajeshi wa Urusi aliyetuhumiwa kwa kumuua mumewe

Muhtasari

• Aliyesimama mahakamani kumkabili mshtakiwa mwenye umri wa miaka 21 siku ya Alhamisi alikuwa Kateryna Shelipova, mjane wa mwanamume aliyeuawa.

• "Utulinde na nani? Umenilinda dhidi ya mume wangu uliyemuua?" Askari huyo alishindwa kujibu.

Mwanajeshi huyo mwenye umri wa miaka 21 alihojiwa nchini Ukraine kupitia mkalimani wa Kirusi
Mwanajeshi huyo mwenye umri wa miaka 21 alihojiwa nchini Ukraine kupitia mkalimani wa Kirusi
Image: EPA

Katika siku za kwanza kabisa za uvamizi huu raia mwenye umri wa miaka 62 ambaye hakuwa na silaha alipigwa risasi kwenye barabara ya kijiji nje ya nyumba yake ya Ukraine. Jina lake lilikuwa Oleksandr Shelipov.

Miezi mitatu baadaye mwanajeshi wa Urusi aliyekamatwa na tuhuma za kumuua yuko mjini Kyiv akihukumiwa kwa uhalifu wa kivita.

Aliyesimama mahakamani kumkabili mshtakiwa mwenye umri wa miaka 21 siku ya Alhamisi alikuwa Kateryna Shelipova, mjane wa mwanamume aliyeuawa.

Je huyu alitubu kosa lake, aliuliza?

Kamanda wa kitengo kimoja cha jeshi la Urusi, Vadim Shishimarin, alijibu kwamba alikiri makosa yake na akaomba msamaha wake. "Lakini ninaelewa hutaweza kunisamehe," aliongeza.

Kateryna Shelipova hakuwa amemaliza. "Niambie tafadhali, kwa nini ninyi [Warusi] mlikuja hapa? Ili kutulinda?" aliuliza, akitoa mfano wa Vladimir Putin anayedai haki ya uvamizi wa Ukraine.

"Utulinde na nani? Umenilinda dhidi ya mume wangu uliyemuua?"

Askari huyo alishindwa kujibu.

'Mume wangu alikukosea nini?' mjane Kateryna Shelipova alimuuliza mwanajeshi wa Urusi ambye alikiri kumuua mumewe.
'Mume wangu alikukosea nini?' mjane Kateryna Shelipova alimuuliza mwanajeshi wa Urusi ambye alikiri kumuua mumewe.
Image: EPA

Kesi hii ya kihistoria inaadhimisha mara ya kwanza kwa mwanajeshi wa Urusi kuwekwa kizimbani kwa uhalifu wa kivita tangu uvamizi wa Ukraine mnamo mwezi Februari.

Na pengine makabiliano hayo yanayohusu majaribio kama haya, angalau kwa sehemu. Kumlazimisha askari - ambaye alipuuza sheria zote za vita - kukabiliana na kile ambacho amefanya na mateso ambayo amesababisha.

Sgt Shishimarin amekiri kufanya makosa na waendesha mashtaka wa Ukraine wanaomba ahukumiwe kifungo cha maisha.

Siku ya Jumatano, Bi Shelipova aliniambia kwa kweli alimhurumia askari huyo, lakini hangeweza kumsamehe kwa uhalifu huu.

Alisikia milio ya risasi iliyomuua mumewe, kisha akamwona Sgt Shishimarin kupitia lango lake - akiwa ameshikilia silaha yake.

Dakika tano baadaye anasema aliuona mwili wa mumewe: "Alikuwa amekufa na risasi kichwani. Nilianza kupiga kelele ."

"Kupoteza mume wangu ndio kila kitu kwangu," Bi Shelipova alisema, na kuongeza: "Alikuwa mlinzi wangu."

'Ilimuua'

Akikumbuka matukio ya tarehe 28 Februari, Vadim Shishimarin alisema yeye na kikundi kidogo cha wanajeshi wengine wa Urusi walikuwa wametenganishwa na kikosi chao na kuteka nyara gari ili kurejea humo.

"Tukiwa tunaendesha gari, tulimwona mwanamume. Alikuwa akiongea na simu," mshtakiwa alisema.

Vadim Shishimarin alizungumza katika mahakama moja mjini kyiv akiwa kizimbani.
Vadim Shishimarin alizungumza katika mahakama moja mjini kyiv akiwa kizimbani.
Image: AFP

Alidai kwamba hakutaka kufyatua risasi , kwamba alikuwa akifuata amri - akitishiwa na askari mwingine iwapo asingefuata amri yake.

"Alisema nitakuwa nawaweka hatarini nisipofanya hivyo. Nilimpiga risasi nikia karibu naye . Ilimuua," kamanda huyo mwenye umri wa miaka 21 aliambia mahakama.

Cha kushangaza ni kwamba wakili wake aliyeteuliwa na serikali - aliniambia kuwa hakuna afisa wa Urusi ambaye amewasiliana naye, hata wizara yake ya ulinzi.

Hakuna ubalozi wa Urusi huko Kyiv siku hizi, kwa hivyo hakuna mawasiliano kutoka huko pia.

Msemaji wa Rais Vladimir Putin jana aliambia BBC kwamba Kremlin "haina habari" kuhusu kisa hicho.

Yote kumi inaonekana kwamba hatma ya askari huyo mchanga iliwachwa kwa makamanda waliompeleka vitani na wanaendelea kukana kwamba vikosi vyao vinafanya uhalifu hapa.

Mwanajeshi wa Urusi aliyekamatwa Ivan Maltysev alikuwa shahidi wa mauaji hayo na alitoa ushahidi mbele ya mahakama
Mwanajeshi wa Urusi aliyekamatwa Ivan Maltysev alikuwa shahidi wa mauaji hayo na alitoa ushahidi mbele ya mahakama
Image: AFP

Pia tulisikia kutoka kwa mwanajeshi wa pili wa Urusi ambaye alishuhudia mauaji hayo mnamo Februari na baadaye kujisalimisha kwa vikosi vya Ukraine.

Ivan Maltysev, kijana mwingine mwenye sura ndogo na mwenye umri wa miaka 21, aliiambia mahakama jinsi wanajeshi wa Urusi walivyomuona Oleksandr Shelipov walipokuwa wakiendesha gari lililoibiwa.

Bw Maltysev alidai kuwa Vadim Shishimarin aliamriwa kumpiga risasi mwathiriwa kwa sababu alikuwa akizungumza na simu .

"Vadim hakufanya hivyo. Kwa hiyo askari, ambaye sijui jina lake, aligeuka ndani ya gari na kupiga kelele kwamba Vadim alipaswa kutekeleza amri hiyo, au tungeigia katika hatari.

"Wakati huu, tulikuwa karibu na raia huyo, chini ya shinikizo, Vadim alifyatua risasi. Alifyatua risasi tatu au nne."