logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais Samia: 'Nimewashinda marais wanaume'

Amesema amesimamia baadhi ya majukumu vyema zaidi kuliko marais wengine wanaume waliomtangulia.

image
na Radio Jambo

Habari26 May 2022 - 02:23

Muhtasari


•Rais Samia Suluhu anasema katika baadhi ya maeneo kwenye majukumu yake ya urais amesimamia vyema zaidi kuliko marais wengine wanaume waliomtangulia

Rais wa Tanzania Samia Suluhu anasema katika baadhi ya maeneo kwenye majukumu yake ya urais amesimamia vyema zaidi kuliko marais wengine wanaume waliomtangulia.Rais wa Tanzania alisema alikabiliwa na changamoto za kutoaminiwa katika siku zake za kwanza ofisini kwa sababu yeye ni mwanamke - jambo ambalo alilazimika kulishinda.

Bi Samia alikuwa akizungumza kwenye kongamano katika mji mkuu wa Ghana Accra – ikiwa ni ziara yake ya kwanza Afrika Magharibi tangu aapishwe kuwa rais kufuatia kifo cha mtangulizi wake John Magufuli Machi 2021.“Ilikuwa vigumu sana kuwafanya watu wa Tanzania kuniamini.

Kwamba naweza kuendesha nchi sawa na wanaume – hiyo ndiyo ilikuwa changamoto kubwa,” alisema wakati wa kikao kilichoandaliwa kama sehemu ya mkutano wa kila mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)."Katika kipindi cha mwaka mmoja nimeonyesha nguvu za wanawake, niliongoza nchi kama wanaume walivyofanya na katika mazingira mengine kwa ubora kuliko wao," aliongeza.

Kiongozi huyo wa Tanzania aliliambia jukwaa la AfDB kwamba ukuaji wa uchumi wa nchi umeshuka kutoka 6.4% hadi 4% wakati wa janga la Covid - lakini chini ya uongozi wake ulipanda hadi 5.2% na ilitabiriwa kufikia 6.7% ifikapo 2025.Kongamano hilo lililofanyika mjini Accra pia lilihudhuriwa na Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na Rais wa Comoro Azali Assoumani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved