Watu wasiojulikana 'waiba makaburi' Msumbiji

Image: AFP

Wakaazi wa mji wa Beira katika jimbo la kati la Msumbiji la Sofala wametaka ulinzi wa makaburi ya eneo hilo huku kukiwa na ripoti za uharibifu wa makaburi. Katika makaburi ya Mangalane, zaidi ya makaburi 50 yameharibiwa katika muda wa mwezi mmoja uliopita.

Wahalifu hao wanaiba misalaba ya shaba na vitu vingine vya chuma. Kiongozi wa kimila anayehusika na makaburi hayo, Fernando Jaime, alisema vitendo vya unajisi vimekuwa vikifanyika mchana kweupe.

"Wanachukua misalaba na vitu vingine vya watu waliokufa wanavyovikuta kando ya kaburi. Wanaweka vitu hivi pamoja na kuviuza kwa chakavu," aliambia vyombo vya habari vya ndani.

Carlos Cassicussa mkazi wa kitongoji cha Mungassa alisema hali hiyo inatokana na kuporomoka kwa maadili. “Hii tabia ni mbayakwa kweli, wizara ya mambo ya ndani ichukue hatua waje makaburini hata saa sita mchana,” alisema.