Mwanamke ajifungua watoto wanne kwa siku tofauti katika kisa cha nadra

Muhtasari

•Siku ya kwanza ya Juni, mwanamke mwenye umri wa miaka 29 alijifungua watoto wanne wasio mapacha - wavulana watatu na mmoja msichana.

Image: BBC

Mwanamke mmoja Croatia amejifungua watoto wanne wakifuatana kwa siku tofauti, hili hutokea mara moja katika miaka kumi, madaktari wanasema.

Ni kisa nadra sana kutokea, kulingana na madaktari, kama wanavyosema, ''muujiza wa Mungu''.

Siku ya kwanza ya Juni, mwanamke mwenye umri wa miaka 29, ambaye hakutaka kuzungumza na vyombo vya habari, alijifungua watoto wanne wasio mapacha - wavulana watatu na mmoja msichana.

Kila mimba ina kondo la nyuma, ambayo, kulingana na madaktari wa Croatia, ni nadra na visa kama hivyo hufanyika mara moja katika miaka kumi.

''Ni mimba ya mayai manne, ambayo ni chaguo bora kwa watoto, bora zaidi kuliko wakati watoto wakiwa katika kondo la nyuma moja,'' alisema Marko Drazen Mimica, mkurugenzi wa Kliniki ya Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Kituo cha Hospitali.

Damir Banovac, babake mwanamke huyo mjamzito, aliambia BBC kwa lugha ya Kiserbia kwamba binti yake anahisi vizuri.

''Ilikuwa nzuri na itakuwa bora zaidi, haswa wakija nyumbani na tunapowaona.''Itakuwa tamu zaidi, tunafurahi, tunafurahi na tunasherehekea, tunaandaa sherehe,'' anasema Banovac kwa uchangamfu.

Watoto wanaozaliwa wana uzito wa kati ya gramu 1,400 na 1,500 na wana urefu wa sentimita 40.

Mara ya mwisho jambo kama hili lilipotokea Croatia ilikuwa katika robo karne iliyopita.

Punde tu wanapokuwa wanne, inakuwa na tukio la ajabu kwa sababu sisi kama viumbe hatutegemewi kuzaa watoto wanne, hivyo mimba hizo ni hatari tangu mwanzo na zinapaswa kufuatiliwa hasa kwa kuzingatia kila kitu ya kimatatibabu hii leo,'' Mimica alisema.

Asingepona kama dawa isingeendelea.

Aliongeza kuwa haingewezekana watoto katika hali hiyo kunusurika kifo kama haingekuwa maendeleo ya kimatibabu hii leo.

'Tunawasubiri kwa hamu kuwaona.'

Kwa muda wa miezi miwili iliyopita, kijana huyu mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akitunza ujauzito wake hospitalini chini ya uangalizi wa kimatibabu.

Alipata mimba kawaida tu na kujifungua kwa njia ya upasuaji.

''Kila kitu kilikwenda sawa,'' alismea baba yake, Damir Banovac.

Anaongeza kuwa hakukuwa na matatizo wakati wa ujauzito pia.

Anajua kwamba hii hutokea mara chache na anadai kwamba yote ni ''mapenzi ya Mungu''.

''Sisi ni familia ya kitamaduni, tuliikubali kama zawadi kutoka kwa Mungu, alitaka iwe hivyo na ndiyo maana yote yalikwenda vizuri,'' anaongeza.

Binti yake ambaye hataki kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari kwa sasa, tayari ana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne, ambaye anatarajia ujio wa kaka na dada zake.

"Walizaliwa mapema, maana yake ni watoto hatari, lakini kwa sasa wanaendelea vizuri na hawana matatizo makubwa," anaeleza Dk.Mimica

Mimba nyingi

Mimba nyingi inamaanisha kuwa kuna kijusi zaidi ya mmoja katika mwili wa mwanamke.

Tukio la kawaida ni mimba za mapacha, ni kawaida kwa mwanamke kuzaa watoto watatu, wakati wanne na watano ni nadra sana.

Watoto watatu hutokea yenyewe mara moja katika mimba 10,000.

Mimba kama hizo kawaida huishia kati ya wiki ya 32 na 34, na uzito wa wastani wa mimba ni karibu gramu 1,800.

Mapacha wanne na mimba zilizo na vijusi watano au zaidi ni nadra sana.

Katika mimba hiyo, ni tabia kwamba kupunguzwa kwa kiinitete katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito inapendekezwa ili kupunguza mimba kwa ni mapacha.

Inafanywa katika kipindi kati ya wiki 10-13.

Mara ambazo mimba hizi hutokea katika nchi nyingi za Ulaya ni kati ya asilimia 0.7 hadi 1.5, lakini hiyo imebadilika sana na maendeleo ya teknolojia.

Sababu kuu zinazoweza kusababisha mimba nyingi ni jeni, kuwepo kwa uterasi mbili na kusitishwa kwa matumizi ya vidonge vya kuzuia mimba.

Inawaathiri zaidi wanawake wenye umri wa kati ya miaka 30 na 35.

* Chanzo: Hospitali Kuu ya Pancevo Nchini Serbia, wanne hao walizaliwa mara ya mwisho miaka minne iliyopita huko Subotica, mji wa kaskazini mwa Vojvodina.

Wenzi wa ndoa Mira na Mladen Krstić walitaka mtoto mwingine na baada ya miaka saba ya kujaribu, waliamua kurutubishwa kwa njia ya utumbo.

"Walirudisha seli tatu na wote watatu walilazwa na awali tulikuwa na watoto watatu, lakini baada ya wiki mbili tuligundua kuwa seli moja iligawanyika na kuwa mapacha wanaofanana na hivyo ndivyo tulivyopata wanne - sote tulipatwa na mshtuko," alisema.

Septemba mwaka jana, Aisha Kilinac (32) kutoka jimbo la Uturuki la Mersin alijifungua watoto wanne.

Anegret Raunigk, 65, alijifungua watoto wanne huko Berlin.

Alipata mimba sio kwa njia ya kawaida, na akajifungua akiwa na wiki 26.

Mnamo Mei 2021, Halima Kisi kutoka Mali alizaa watoto tisa na akaingia Kitabu cha Rekodi cha Guinness.

Alijifungua huko Morocco, na kabla ya kujifungua, uchunguzi wa ultrasound ulionyesha kwamba alikuwa amebeba watoto saba.

Mwanzoni mwa Mei 2022, wale tisa walisherehekea siku yao ya kuzaliwa ya kwanza, na baba yao alisema kwamba watoto walikuwa ''wenye afya kama kulungu''.