Mwanamume awashtaki wazazi wake kwa kumzaa

Muhtasari

•Raphael Samuel ambaye ni mfanyabiashara amesema kuwa haikuwa sahihi kuleta mtoto duniani na kuishia matatizoni maisha yake yote.

Mwanamume awashtaki wazazi wake kwa kumzaa
Mwanamume awashtaki wazazi wake kwa kumzaa
Image: NIHILANAND

Mwanamume wa miaka 27 wa India anapanga kuwashtaki wazazi wake kwa sababu hawakuomba ridhaa yake ili azaliwe.

Raphael Samuel, mfanyabiashara mwenye makazi yake Mumbai, aliambia BBC kuwa haikuwa sahihi kuleta mtoto duniani na kuishia matatizoni maisha yake yote.

Anaelewa kuwa haiwezekani kuuliza maono kutoka kwa mtu ambaye hajaja ulimwenguni, lakini anasisitiza ‘’uamuzi wetu sio kuzaliwa’’.

Hatua hiyo inaweza kusababisha mabishano katika familia yoyote, lakini inaonekana familia yake inaifanyia mzaha.

Katika taarifa iliyotolewa na mamake Kavita Karnad Samuel alisema alimpongeza mwanawe kwa kumpeleka mahakamani, akijua kuwa wote ni mawakili.

Samuel anaomba mahakama iamuru alipwe fidia na wazazi wake.

Wazo la mtu huyu linatokana na mtazamo wa kifalsafa kwamba maisha ni magumu, na kwa hiyo ametelekezwa