Umoja wa Mataifa wahimiza hatua za haraka kuepusha njaa nchini Somalia

Muhtasari

•Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu Adam Abdelmoula amesema jumuiya ya kimataifa lazima ichukue hatua sasa au watu zaidi watakufa

•Mifugo milioni tatu, ambayo ni chanzo kikuu cha maisha, wamekufa kutokana na ukame.

Mifugo milioni tatu wamekufa kutokana na ukame.
Mifugo milioni tatu wamekufa kutokana na ukame.
Image: BBC

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa Somalia inaelekea kwenye baa la njaa huku nchi hiyo ikikabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika takriban miongo minne.

Kwa sasa, karibu nusu ya watu wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini humo, Adam Abdelmoula, amesema jumuiya ya kimataifa lazima ichukue hatua sasa au watu zaidi watakufa.

Alisema nchi iko kwenye ukingo wa njaa mbaya na iliyoenea na njaa kubwa ambayo inaweza kuchukua mamia ya maelfu ya maisha.

Misimu minne ya mvua mfululizo imeshindwa na Umoja wa Mataifa unakadiria ukame mkali uliofuata umeathiri watu milioni saba na wengine zaidi ya 800,000 kuyahama makazi yao.

Wakati huo huo, bei ya vyakula inapanda kwa kiasi kwa sababu ya vita nchini Ukraine - na usaidizi wa kibinadamu haupatikani kwa wengi kwa sababu ya ukosefu wa usalama na migogoro.

Mifugo milioni tatu, ambayo ni chanzo kikuu cha maisha, wamekufa kutokana na ukame. Bw Abdelmoula alisema mwitikio kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kufikia sasa haujatosha.

.Mnamo 2011, ukame mkali ulisababisha njaa ambayo iliua watu robo milioni.