Kenya kuanza tena mauzo ya miraa Somalia

Muhtasari
  • Alisema mazungumzo ya kibiashara yalitiwa nguvu baada ya wajumbe wa Kenya wakiongozwa na Rais Kenyatta kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Bw Sheikh mjini Mogadishu Alhamisi

Serikali ya Somalia imeondoa marufuku ya miaka miwili ya usafirishaji wa miraa kutoka Kenya, kufuatia mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Rais Uhuru Kenyatta na rais mpya wa nchi hiyo Hassan Sheikh Mohamud Alhamisi.

Waziri wa Kilimo Peter Munya alisema usafirishaji wa zao hilo linalokuzwa Meru utaanza baada ya wiki mbili ambapo wakuu hao wa nchi watatia saini makubaliano rasmi ya kibiashara.

Bw Munya alitangaza kuwa safari za ndege za moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili pia zitaanza tena kuanzia Jumanne ijayo katika hatua ambayo itawezesha zao hilo kusafirishwa moja kwa moja kutoka uwanja wa ndege wa Isiolo.

Akihutubia wanahabari nje ya zahanati moja katika Kaunti ya Meru alipoanza ziara ya siku mbili ya kikanda kwa wakulima wa eneo hilo, Bw Munya serikali mpya ya Somalia ilikuwa imeahidi kuboresha uhusiano wa kidiplomasia.

Alisema mazungumzo ya kibiashara yalitiwa nguvu baada ya wajumbe wa Kenya wakiongozwa na Rais Kenyatta kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Bw Sheikh mjini Mogadishu Alhamisi.

"Tunataka kumshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa mazungumzo ya kidiplomasia ambayo amekuwa akifanya kimya kimya.

Marufuku hiyo ilikuwa imeathiri pakubwa uchumi wa Mlima Kenya Mashariki na mapato ya wakulima," akasema.

Bw Munya alisema mazungumzo yamekamilika na kilichosalia ni kutia saini makubaliano katika mkataba ambao utaifanya Somalia kuiuzia Kenya vyakula vya baharini na mazao mengine.

Bw Munya alisisitiza umuhimu wa soko la Somalia akisema ndilo lililokuwa na faida kubwa zaidi na lilitumika kama sehemu ya kuzindua usafirishaji mizigo kuelekea Pembe ya Afrika, Mashariki ya Kati na mataifa mengine.

Waziri pia alisema kuwa visa vitarahisishwa kwa Wasomali wanaokuja Kenya.

Serikali ya Farmajo ilisitisha safari za ndege kuelekea Kenya mnamo mwaka 2020 kutokana na maambukizi ya Covid-19, lakini marufuku hiyo haikuondolewa kwa sababu ya mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Somalia ndio soko kubwa zaidi la kuuza mirungi nchini Kenya na angalau safari 16 za ndege kila siku zilikuwepo kubeba mirungi kwenda Somalia kabla ya kuwekewa vikwazo.

Marufuku hiyo ni pigo kwa biashara ya mirungi nchini Kenya, ambayo inarejea kutokana na athari za serikali ya Uingereza kupiga marufuku usafirishaji wake nje ya nchi kwa vile inatambua kuwa dawa.

Hata hivyo, Somalia bado haijatoa maoni yoyote kuhusu makubaliano hayo yaliyotangazwa na serikali ya Kenya.

Athari iliyojitokeza ya marufuku

Wakati nchi nyingi ilijikuta zinasimamisha shughuli za kibiashara kwasababu a ugonjwa wa corona wafanyabiashara wengi kutoka Kenya waliathirika kwasababu walilazimika kusitisha biashara ambayo waliitegemea katika kukimu mahitaji yao ya kila siku.

Karibu wakulima nusu milioni wanaolima kichocheo hicho katika upembe wa Afrika, ,wengi wao wataathiriwa na marufuku.

Na pia, watafunaji, kuna wengi walioathirika kama Bwana Mohamed Abdi.

"Mwanaume bila miraa ni kama samaki nje ya maji ," anasema Mohamed Abdi mtafunaji maarufu mjini Mogadishu. "Nanapenda sana . Lakini siwezi kuhimili kupanda kwa bei yake, kwa hiyo ninakuwa kama nimechanganyikiwa."

"Nimeacha kutafuna mirungi kwa sababu ya bei yake kubwa," anasema mtafunaji mwingine, Hassan Abdiwali. "Baadhi ya marafiki zangu wameanza kutumia vitu vingine kama dawa haramu au pombe zinazotekenezwa nyumbani . Wengine wameanza wizi ili waweze kununua mi