Morocco yaripoti kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Monkeypox

Muhtasari

•Mtu aliyeambukizwa ana historia ya kusafiri kwenda Ufaransa na ametengwa, kulingana na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).

Dalili kubwa ya ugonjwa wa monkeypox ni upele mbaya na wenye matuta
Dalili kubwa ya ugonjwa wa monkeypox ni upele mbaya na wenye matuta
Image: BBC

Morocco imeripoti kisa chake cha kwanza cha ugonjwa wa monkeypox kilichothibitishwa, nchi ya kwanza isiyo na ugonjwa huo barani Afrika kufanya hivyo.

Mtu aliyeambukizwa ana historia ya kusafiri kwenda Ufaransa na ametengwa, kulingana na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).

Mwishoni mwa Mei, kituo cha CDC Afrika kilisema wale ambao walipima virusi vya ugonjwa huo katika bara hili hawakujulikana kuwa walisafiri nje ya nchi kabla ya kuambukizwa.

Kunganisha usafiri hadi Ufaransa kuna hitaji uchunguzi wa kina zaidi na mpangilio katika bara hilo.

Wakati wa mkutano wake wa kila wiki, Dk Ahmed Ogwell, kaimu mkuu wa Afrika CDC, alisema kuwa ingawa ugonjwa wa monkeypox unaenea kimataifa, uingiliaji kati wowote, na mipango yoyote ya kudhibiti virusi vya ugonjwa huo, inapaswa kuanza barani Afrika.

‘’Mahali pa kuanzia chanjo inapaswa kuwa Afrika na sio kwingineko,’’ alisema.