Papa Francis aahirisha ziara yake nchini DR Congo na Sudan Kusini

Muhtasari
  • Papa Francis aahirisha ziara yake nchini DR Congo na Sudan Kusini
pop
pop

Papa Francis amelazimika kukatiza ziara yake ijayo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini kwa sababu ya jeraha la goti, Vatican imetangaza.

Mkuu wa Kanisa Katoliki alipangiwa kusafiri mwezi Julai hadi miji ya Kinshasa na Goma ya Kongo, ikifuatiwa na ziara katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba. Huko Juba alipaswa kuongoza mkesha wa maombi pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby, na

Msimamizi wa Mkutano Mkuu wa Kanisa la Presbyterian la Scotland Mchungaji Iain Greenshields. Vatican ilisema ziara hiyo itafanyika katika "tarehe ya baadaye kuamuliwa".

Uamuzi huo ulikuwa umefanywa "kwa ombi la madaktari [wa Papa], na ili kutohatarisha matokeo ya matibabu ambayo anapitia kwa goti lake". Baraza la Maaskofu Katoliki Sudan na Sudan Kusini bado halijatoa tamko lolote kuhusu kuahirishwa.

Nchi za DR Congo na Sudan Kusini zina idadi kubwa ya Wakatoliki wa Kirumi. Papa huyo mwenye umri wa miaka 85 amefanya ziara kadhaa barani Afrika tangu kuwa papa mwaka 2013.