Akina mama wa Urusi wanawasaidia wanao ambao hawataki kupigana

Muhtasari

•Kamati ya Akina Mama wa Wanajeshi, inayofanya kazi ya “kulinda haki za wanajeshi,” inasema imekuwa ikisaidia familia za Warusi zinazopinga vita.

•Kumekuwa na madai kwamba wanajeshi wa Urusi wanakataa kurudi vitani kwa kupelekwa kwa mara ya pili - au hawatapigana kabisa .

Image: BBC

BBC iliripoti juu ya ukosoaji wa Papa Francis kwa wanajeshi "wakatili " wa Urusi - na Rais Zelensky wa Ukraine akilaani vitendo vya jeshi la Urusi kama "maovu kabisa".

Lakini pia kumekuwa na madai kwamba wanajeshi wa Urusi wanakataa kurudi vitani kwa kupelekwa kwa mara ya pili - au hawatapigana kabisa .

Kamati ya Akina Mama wa Wanajeshi, inayofanya kazi ya “kulinda haki za wanajeshi,” inasema imekuwa ikisaidia familia za Warusi zinazopinga vita.

Katika mahojiano na chombo cha habari cha Urusi Meduza, katibu mtendaji wa shirika hilo lisilo la kiserikali Valentina Melnikova alisema baadhi ya watumishi wanaoondoka Ukraine wameomba ushauri wa kamati ili kuepuka kurudi kwenye mstari wa mbele.

Dk Jenny Mathers, msomi katika Chuo Kikuu cha Aberystwyth ambaye anasoma Ukraine, alisema kuongezeka kwa wanajeshi wasiotaka kupigana kunaweza kuwa na athari kubwa.

"Uwezo wa Urusi sio usio na mwisho," alisema.

"Tuna visa zaidi na zaidi vya wanajeshi wa Urusi ambao wamehudumu nchini Ukraine na kurudi Urusi wakikataa kurejea tena kwa kutumwa vitani.

"Tuna mifano zaidi na zaidi ya ofisi za kuandikisha jeshi la Urusi kushambuliwa, kuteketezwa ... hadithi zaidi na zaidi za familia zilizo tayari kusaidia wana wao wanaojificha kutoka kwa jeshi."

Ingawa BBC haiwezi kuthibitisha madai yote ya Mathers, hivi majuzi tuliripoti kuhusu wanajeshi wa Urusi waliokataa kupigana nchini Ukraine.

Urusi na Ukraine: Papa akosoa matumizi mamluki wa 'kuogofya ' ya Urusi

Image: BBC

Papa Francis: ’Vita ya III ya Dunia tayari imetangazwa’

Pope Francis ameripotiwa akisema kuwa matumizi ya mamluki wa Uusi nchini Ukraine, wakiwemo Wachechnya na Wasyiria ni "ya kuogofya" katika Makala iliyochapishwa na gazeti la kila siku la Italia, La Stampa.

Katika kipande, ambacho huripoti mazungumzo kati ya Papa na Mhariri wa jarida la utamaduni la Jesuit European, Papa alisema kuwa Vita vya Ukraine ni vya "labda nia ya kuchokoza kwa njia moja au sio vya kuiwa".

Aliyaelezea majeshi ya Warusi kama majeshi "makalik na katili", akiongeza kuwa Waukraine wana "pigana kwa ajili ya kuishi".

Alipoulizwa iwapo anampenda Rais wa Urusi, Vladimir Putin, Papa Francis anasema hatapunguza ugumu wa vita kwa kutofautisha"wema na ubaya".

Aliendelea kusema kuwa ana matumaini ya kukutana na- Mkuu wa Kanisa la Waorthodox wa Urusi Patriarch Kirill mwezi Septemba nchini Kazakhstan